Tuesday, October 23, 2012

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA ILI KUEPUKANA NA HASARA MBALIMBALI


Na Queen Lema, Arusha 

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA ILI KUEPUKANA NA HASARA MBALIMBALI

Nchi za Afrika zimetakiwa kuhakikisha kuwa zinajiwekea utaratibu wa kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vya hali ya juu sana ili kuweza kujiepusha na hasara zinazotokea kwenye ukaguzi, pamoja na kwenye masoko mbalimbali ya uuzaji wa bidhaa hizo.

Hayo yameelezwa mjini hapa na kaimu mkurugenzi mkuu shirika la viwango Tanzania(TBS)Bw Leandri Kinabo wakati wa mkutano  wa baraza la utendaji  la mashirika ya viwango Afrika linaloshirikisha nchi 11 (ARSO)unaendelea mjini hapa

Bw Kinabo alisema kuwa nchi za Afrika zinatakiwa kuhakikisha kuwa zinakuwa marafiki wazuri wa kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vya hali ya juu sana kwani uzalishaji wa bidhaa ambazo hazina ubora ni chanzo kikubwa sana cha hasara hasa kwa wenye viwanda na kwa watumiaji wenyewe.

Alifafanua kuwa bidhaa zenye ubora zinachangia sana maendeleo ya Nchi na Bara jambo ambalo kila mdau anatakiwa kuhakikisha kuwa anafuata taratibu na sheria za uzalishaji bora ili kuweza kuraisisha hata biashara zao tofauti na pale ambapo bidhaa zinakosa ubora ambao unaitajika

“kama nchi za bara la afrika na Tanzania itaweza kuzalisha bidhaa zenye ubora ni wazi kuwa wataweza kuchochea sana maendeleo kwa kuwa hata biashara nazo zitaweza kukua na kuimarika zaidi kwenye ubora wa hali ya juu lakini kama watakuwa wanakwepa njia mbalimbali za uzalishaji bora basi watachangia sana umaskini hasa wan chi hizi ingawaje kuna rasilimali nyingi sana”aliongeza bw Kinabo

Katika hatua nyingine alifafanua kuwa ili kuboresha zoezi hilo la ubora wa bidhaa hasa kwa nchi za Afrika wataweza kujadili masuala mbalimbali ambayo yataweza kufanya nchi zote kutumia kiwango kimoja cha ubora tofauti na pale ambapo kila nchi inapotumia viwango vyake vya ubora.

Alisema kuwa kupitia utaratibu huo wa kutumia viwango vinavyofanana  kwa nchi zote za Afrika wadau mbalimbali hususan wafanyabiashara wataweza kuepukana na vikwazo mbalimbali ambavyo vinachangia sana kukwamisha malengo yao mbalimbali kutokana na Ubora wa bidhaa kwa nchi husika

“ndani ya baraza hili tutaweza kuweka utaratibu maalumu wa kuhakikisha kuwa tunatumia viwango ambavyo vinafanana na hii itasaidia sana kuweza kuharakisha maendeleo kwa bidhaa na biashara mbalimbali tofauti na pale ambapo kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa viwango lakini njia hii ni raisi sana hivyo tutawekeana mikakati mbalimbali ya kuhakikisha hilo linaboreshwa”aliongeza bw Kinabo


Alimalizia kwa kusema kuwa nao wananchi wa Tanzania wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kutumia na kuimarisha zaidi bidhaa ambazo zina ubora wa hali ya juu kwani kwa kutotumia bidha ambazo hazina nembo ya shirika la viwango nchini  pamoja na ubora unaoitajika na Serikali ni chanzo cha madhara makubwa sana kwa watumiaji wa bidhaa 

No comments:

Post a Comment