Friday, October 19, 2012

TANZANIA KUENDELEA KUBORESHA HIFADHI ZA UTALII PAMOJA NA VYANZO VYA MAZINGIRA

Na Queen Lema, Arusha

TANZANIA KUENDELEA KUBORESHA HIFADHI ZA UTALII PAMOJA NA VYANZO VYA MAZINGIRA

SERIKALI ya Tanzania imesema kuwa itaendelea kuweka na kuimarisha mikakati mbalimbali ya mazingira pamoja na utalii ambapo mikakati hiyo itaenda sambamba na kuzuia makazi ya watu karibu na vyanzo mbalimbali vya mazingira na hifadhi kwani makazi hayo ni tishio kubwa sana kwa wanyama

Hayo yameelezwa na Makamu wa Raisi Dkt Gharib Bilal wakati akifungua Kongamano la kwanza la usimamizi endelevu katika hifadhi za taifa mapema leo jijini hapa

Dkt Bilal alisema kuwa mikakati hiyo itafanya baadhi ya wananchi kushindwa kukaa karibu na vyanzo na hifadhi za wanyama kwa kuwa asilimia kubwa ya makazi ya watu yamekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira pamoja na vifo vya wanyama hasa Tembo hali ambayo inafanya malengo mbalimbali ya uhifadhi kushindwa kutimia

Aliongeza kuwa pamoja na kuweka mikakati hiyo lakini bado suala hilo limekuwa ni gumu sana kwa wananchi kwa kuwa baadhi ya wananachi ambao wanafukuzwa katika vyanzo  vya mazingira wanagoma kuondoka huku idadi ya wanyama nayo ikiwa inapungua kutokana na makazi hayo

“tuna mikakati ya kuhakikisha kuwa maeneo ya hifadhi ya taifa  na vyanzo vingine vya mazingira vinahifadhiwa na kamwe maeneo haya yasiingiliwe kwa ajili ya makazi ya kudumu ya watu ambapo kama tutafanikiwa kufanya hivi basi tutachangia sana kwa kiwango kikubwa  kuongeza hata idadi ya wanyama hasa Tembo ambao wamepungua sana ndani ya hifradhi mbalimbali za Taifa hapa nchini”aliongeza Dkt Bilali

Awali Naibu katibu mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohuisiana na utalii(UNWTO)bw Hifad Twalib  alisema kuwa utalii unatakiwa kuanzia ngazi ya chini na endapo kama wananchi wa nchi husika hawafurahii utalii basi utalii huo utakuwa hauna maana halisi hasa kwenye mapato.

Aliwataka wananchi wan chi zote hasa kwa bara la Afrika kuhakikisha kuwa wanayafuraia mazingira ya utalii na kuhakikisha kuwa wanakuwa mabalozi wazuri hali ambayo kama itafanikiwa kuboreshwa basi hata idadi ya vyanzo mbalimbali vya utalii navyo vitaongezeka kwa kuwa baadhi ya vyanzo vya utalii vinakufa kwa kuwa hakuna uhamasishaji mkubwa.

‘sasa unakuta nchi inatangaza utalii wakati wananchi wake wenyewe hawajui  na kwa kweli hili ni suala gumu sana wananchi wanatakiwa kubadilika na kuhakikisha kuwa kabla ya wageni kutoka nje ya nchi hawajaja wananchi wenyewe waweze kuutambua na kuthamini utalii nah ii itasababisha sana wananchi kuweza kunufaika sana na hata kuutangaza utalii wao wenyewe’aliongeza

MWISHO

No comments:

Post a Comment