Thursday, October 11, 2012

ACHENI MATAMBO YA KWENYE ANASA NA SHEREHE CHANGIENI ELIMU-SARAKIKYA



Na Queen Lema,Meru

VIONGOZI mbalimbali wa siasa, wazazi pamoja na walezi wameombwa kuwekeza nguvu zao zaidi katika elimu na kuachana na tabia ya kuwekeza zaidi katika anasa, na sherehe mbalimbali huku sekta hiyo ikikabiliwa  na changamoto kubwa sana za uhaba wa vyumba vya madarasa, pamoja na uhaba wa mabweni huku hivyo vikiwa ni vikwazo vya kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu

Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni Wilayani Meru na Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Meru,Bw William Sarakikya alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuongeza vyumba vya madarasa kwa shule ya Sekondari ya Unambwe .

Alisema kuwa Changamoto ambazo zipo kwenye shule za Sekondari ndani ya Wilaya hiyo ni nyingi sana ingawaje wilaya hiyo ni moja ya wilaya yenye wadau wengi sana wakiwemo wana siasa ambao mara kwa mara wanachangia Sherehe mbalimbali tena kwa kutambiana sana kwa kuwa na fedha nyingi sana.

Aliongeza kuwa matambo ambayo yanatumika na wadau hao mbalimbali wakiwemo wanasiasan yanatakiwa kutumika ndani ya  shule mbalimbali kwa kuhakikisha kuwa shule hizo zinakuwa na maitaji muhimu sana kwani Elimu ni Urithi ambao ni wa kudumu tofauti na sherehe pamoja na anasa za dunia.

“unapochangia sherehe unakula unasahau lakini kama tutaoneshana ubabe wetu hasa sisi wanasiasa kwa kushika shule ambazo zinatuznguka na kuanza rasmi Harambee basi tutachangia kwa kiwango maendeleo ya shule hasa kwa kipindi hiki ambacho kina umuhimu mkubwa sana wa kuwa na mabweni hasa upande wa wanafunzi wa kike”aliongeza

Pia alisema kuwa nao wazazi hasa wa Wilaya hiyo ya Meru wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawapa watoto fursa ya kupata elimu bora kwa kuhakikisha asilimia kubwa ya wanafunzi wanakaa Bweni ili kuweza waweze kupata muda wa ziada wa kujisomea mashuleni tofauti na wanapokuwa majumbani mwao.

“Nawasihi sana wazazi wenzangu hakikisheni hii wilaya inakuwa ni moja ya wilaya yenye mabweni mengi sana ili hawa watoto wetu waweze kupata muda wa ziada wa kujisomea tofauti n pale ambapo wanapokaa majumbani mambo yanakuwa ni mengi sana  hivyo kusababisha wanafunzi wetu kukosa hata muda wa kujisomea huku hali hiyo ikisababisha mdondoko wa elimu”aliongeza Bw Sarakikya.

Awali,Wanafunzi wa shule hiyo ya Unambwe walisema kuwa ili waweze kufanya mithiani yao ya mwisho vema ni lazima changamoto za msingi ziweze kutatuliwa kwani wapo wanafunzi ambao wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika masomo lakini wanakwamishwa na changamoto hizo.

Walitaja Changamoto hizo ambazo ni kikwazo pekee cha kuwafanya washindwe kufikia viwango bora vya kufaulu kuwa ni pamoja na changamoto ya uhaba wa madarasa, uhaba wa walimu,uhaba wa vifaa kwa ajili ya maabara hali ambayo ni chanzo cha ongezeko kubwa sana la Mbumbumbu ndani ya Taifa la Leo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment