Monday, October 15, 2012

WAZEE ZAIDI YA 500 KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI ARUSHA


WAZEE ZAIDI YA 500 KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI ARUSHA

Na Mery Kitosio, Arusha

ZAIDI ya wazee 500 kutoka katika kata za Sombetini,Elerai,na Sokoni one Jijini Arusha wanatarajiwa kunufaika na elimu ya ujasiamali kutoka katika shirika binafsi  la Inform Sector Team (INSET) ambapo wazee hao wataweza kuanzisha miradi mbalimbali  ndani ya jamii zao na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi wa kila kitu.

Akiongea na “Jambo leo’  mjini hapa mapema jana mara baada ya kuwapa semina hiyo  baadhi ya wazee  wa kata hizo tatu Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Japhet Sauni alisema kuwa mpango huo tayari umeshaanza kutekelezwa kwa baadhi ya wazee  na lengo halisi ni kuachana na  umaskini ambao unasababisha Umaskini mkubwa

Japhet alisema kuwa shirika hilo limeamua kufikia uamuzi huo mara baada ya kuona kuwa asilimia kubwa sana ya wazee wanapata shida ndani ya jamii zao kwa kuwa hawana vipato vya kutosha huku hali hiyo ikisababisha baadhi yao kufa kabla ya wakati na kuacha familia zao zikiwa Yatima.

Aliongeza kuwa Uamuzi huo wa shirika hilo la kuwapa wazee hao 500 elimu ya ujasiamali utaweza kuwasaidia kubuni biashara mbalimbali ambazo zitaweza kuwanufaisha na kuwafanya waweze kujimudu katika maisha yao ya kila siku sanjari na kuweza kujihudumia katika maitaji ya msingi ambayo yanakosekana katika familia zao.

“leo unakuta mzee anakaa tu nyumbani anasubiri kuomba omba na kupewa vyakula na watoto wao lakini pindi hawa watoto wanapokosa riziki hawa wazee wanaaza kuandamwa na magonjwa kwa kuwa hawana  hata vyakula lakini kama wakianza kuwa wajasiamali wa biashara ndogondogo basi watachangia sana kuondokana na umaskini ambao umekithiri sana kwenye maisha ya baadhi ya wazee wa leo  kwa kuwa baadhi yao bado wanaonekana kuwa na nguvu kubwa ya kuweza kuendeleza biashara mbalimbali lakini bado hawana elimuy ya kutosha ’aliongeza.

Pia alisema kuwa mara baada ya wazee hoa kuweza kupatiwa elimu ya ujasimali ambayo imeanza kutolewa kwa wazee hao kuanzia sasa wataweza kuanzisha miradi mbalimbali ambapo kupitia miradi hiyo wataweza  kujiunga na Chama cha   kuweka na kukopa cha wazee hali ambayo nayo itaweza kuboresha sana maisha ya wazee hasa wa Jiji la Arusha.

‘tunachokiitaji hapa ni wazeee hawa wainuke na waachane na tabia ya kuwa tegemezi zaidi,na kama wakishapata elimu hii ya ujasiamali bado shirika halitaweza kuwaacha badala yake tunawapa mbinu mbalimbali za kuboresha miradi baada ya hapo sasa tunawapeleka katika Saccos ya wazee na mpaka kufika hapo tunakuwa tumewasaidia wazee hawa kwa kiwango cha hali ya juun sana tofauti na pale kama tungewaacha kwenye jamii zao’aliongeza Japheti.

Alimalizia kwa kusema kuwa wazee wa Kitanzania hawapaswi kukata tama ya maisha kwa kuwa  wana umri mkubwa sana badala yake wanatakiwa muda ambao wanakaa majumbani mwao kuweza kuutumia kiujasimali ambapo kama watafanya hivyo basi watachangia sana hata baadhi ya Vijana nao kuweza kuimarisha uchumi wao wa kila siku.

MWISHO

No comments:

Post a Comment