Tuesday, October 23, 2012

MAJIRA YA KILIMO HASA UPANDAJI NA UVUNAJI ASILIMIA KUBWA YA WAKRISTO WANAKWEPA MAKANISA YAO


MAJIRA YA KILIMO HASA UPANDAJI NA UVUNAJI ASILIMIA KUBWA YA WAKRISTO WANAKWEPA MAKANISA YAO.

Na Bety Alex, MERU

MAKANISA ya pembezoni mwa miji na ndani ya Vijiji mbalimbali kwa mkoa wa Arusha yanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na waumini wachache sana hasa katika majira ya Upandaji na Uvunaji hali ambayo inasababisha Mipango mbalimbali ya makanisa hayo kukwamaa

Asilimia kubwa ya wakristo hasa maeneo ya Vijijini wanashindwa kuhudhuria nyumba za ibada kwa misimu kama ya kilimo huku hali hiyo ikisababisha baadhi yao kushindwa kusonga mbele zaidi katika masuala ya kiroho na kukwamisha shuguli mbalimbali za kanisa.

Changamoto hiyo imeeelezwa na Mchungaji William Ayo wa kanisa la AMEC,usharika wa kileleni Kikatiti Wilayani Meru mkoani hapa wakati akizungumza katika Harambee ya ujenzi wa kanisa  hilo iliyofanyika kanisa hapo wiki iliyopita.

Alisema kuwa makanisa hayo ya Vijijini tena yaliyo mengi sana yanakosa hata waumini kwa nyakati kama hizo ambapo asilimia kubwa sana ya wanaelekea kwenye nyakati za kulima na kufuga huku Mungu naye akiwekwa kando mpaka mazao yatakapovunwa

Alibainisha kuwa hali hiyo ni hatari sana kwa maisha ya kiroho kwani muda na nyakati kama hizo shetani anatumia mwanya huo kuchukua mali zake na kusababisha madhara makubwa sana kwa jamii wakati kwa wale ambao wanaamini kwa majira yote wanaweza kuwa huru zaidi.

“asilimia kubwa sana ya watu wanaumiza akili zao na mawazo mengi sana kuwaza juu ya vitu vya dunia na kuacha kumuwaza zaidi Mungu kwani wakati wa kilimo wengi wanawaza kupatra mazao mengi zaidi kuliko kumuwaza Mungu aliyejuu na hii inachangia sana hata makanisa mengi sana kuweza kushinda kutekeleza mipango yake mbalimbali ambayo wamejikea kwa kuwa hakuna watu wanakuja katika nyumba za ibada kwa misimu pekee”aliongeza

Katika hatua nyingine aliongeza kuwa nayo makanisa ya Vijijini yanatakiwa kuacha kukata tamaa juu ya kuwaombea watu wake ambao wanawaza na kutumia zaidi muda wao katika kutafakari majira ya Mwaka na badala yake wahakikishe kuwa wanawaombea na kwenda kuwaleta kwani wakiwa nje ya kundi kwa ajili ya Kilimo wanakuwa na muda mzuri wa kumtumikia zaidi Shetani kuliko Mungu

Hataivyo aliongeza kuwa nao wadau mbalimbali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea hata tabia ya kuchangia makanisa ya Vijijini kwani asilimia kubwa ya watu wanachangia zaidi makanisa ambayo yapo Mijini kuliko yale ambayo yapo Vijijini ambapo ndipo kwenye uitaji mkubwa sana kutokana na hali ngumu ya maisha ambayo inafanya baadhi ya watu kwenda makanisani kwa msimu

Awali katika harambee hiyo vifaa mbalimbali vya ujenzi vilipatikana sanjari na kiasi cha zaidi ya Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo la Amec wilayani Meru Mkoani hapa.

MWISHO

No comments:

Post a Comment