Friday, October 19, 2012

ACHENI MADHABAU ZA MABABU NA MABIBI ILI MUACHANE NA UMASKINI NA MATESO YA DUNIA

ACHENI MADHABAU ZA MABABU NA MABIBI ILI MUACHANE NA UMASKINI NA MATESO YA DUNIA

Na Bety Alex,ARUSHA

MCHUNGAJI Mary Andrew wa kanisa la Victory Gospel Centre liliopo Oltulelei Jijini hapa amesema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao wanalia na umaskini katika maisha yao ila bado hawajajua kuwa chanzo cha umaskini ambao wanao ni madhabau mbalimbali ambazo walishawahai kuzitumikia au wanazozitrumikaia kwa sasa

Hili suala la Madhabau halibagui wala halichagui  mtu yoyote yule anaweza kuyatumikia hata kama ameokoa ili hali kama hajavunja na kuyakata madhabau mbalimbali ambayo yanaendelea hapa duniani

Mchungaji Maria aliyasema hayo wiki iliyopita wakati akionmgea na waumini wa kanisa hilo kuhusu umuhimu wa kukataa  kutumikia miungu miwili ambayo ni kanisa pamoja na madhabau

Aidha alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao kila siku wanalia nakuomba kukataa  maroho mbalimbali huku wakiwa wanatumia madhabau nyingine katika kuweka imani hali ambayo inawafanya walio wengi sana kuwa maskini

Alifafanua kuwa hali hiyo ya kutegemea zaidi madhabahu kuliko Mungu ndio inayochangia kwa kiwango kikiubwa sana watu wa leo kukosa haki zao za msingi kutoka kwa Mungu kwa kuwa imani zao zimejengeka zaidi katika imani za kimadhabu kuliko kwa Mungu ambaye ndiye tegemeo kubwa sana

‘ndani ya makanisa mpaka watu wanaokoka na wanakiri kabisa kumwamini kristo lakini nyuma ya mapazia wanakuwa wanamuamini zaidi vibabu hasa kwenye madhabau sasa hii ndio inayopelekea walio wengi sana kuwa na mateso mbalimbali ikiwemo roho ya umaskini ambayo inatembeea sana katika maisha ya wakristo hivyo nawasihi sana kuweza kubadilika”alkiongeza Mchungaji huyo

Katika hatua nyingine alisema kuwa wale wanaotumia madhabahu mbalimbali wanakuwa katika ulimwengu miwili tofauti kwa kuwa
Kuwa madhabau hizo zinawaunganisha watu na kuzimu ambapo ndipo kwenye chanzo kikubwa sana cha mateso ya leo hapa duniani

‘biblia inaonesha hivyo kabisa kuwa zipo baadhi ya madhabau ambazo zinaunganishwa na kuzimu  na hizi madhabau zimejengwa na mababu na mabibi sasa sisi watoto wa leo tunaoibukia huko ndio tunaopata matatizo, majeraha, na mateso ya kudumu tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaacha madhabahu hizo na kuangalia Kitabu cha Mithali 12 ambacho kinasema na kudai kuwa Mungu hana upendeleo kwa yeyote yule ambaye anamtegemea”aliongeza

Alimalizia kwa kusema kuwa makanisa ya leo yanatakiwa kuongeza na kuimrasisha nguvu zaidi katika kuwafundisha wakaristo wake umuhimu wa kuyakimbia madhabahu na endapo kama makanisa hayatweza kufanya hivyo basi yatakuwa yanachangia sana  mateso na manunguniko makubwa sana kwa maisha ya kila siku.

MWISHO

No comments:

Post a Comment