Sunday, October 7, 2012

CCM WAZINDUA KAMPENI ZAKE ZA UDIWANI KATA YA DARAJA MBILI

 Na Mustapha Leu, ARUSHA

CHAMA cha mainduzi, wilaya ya Arusha kimewaomba wananchi wa kata ya Daraja mbili jijini Arusha kumuunga mkono mgombea wa CCM, kwenye nafasi ya udiwani .Philip Mushi, katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Oktoba 28 mwaka ili aweze kukamilisha miradi iliyoaachwa na aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu, Bashiri Msangi.

Akizindua kamempeni za uchaguzi mdogo katika mtaa wa Ally Nyanya,  Oktoba 6,sanjari na kumnadi mgombea , mwenyekiti wa CCm, wilaya ya Arusha, Dakta Wilfred Soileli, amesema Philip Mushi ni mtu anayekubalika na ndie atakawezesha kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maendeleo na kazi yake ni ubunifu .

Akawataka wanachama wa CCm, kutokujibizana mitaani na vyama vya kisiasa bali majibizano yafanyike kwa kumchagua ,Mushi ,kuwa diwani wa kata hiyo ili aweze kukamilisha miradi iliyobakia na  kuwaondolea wananchi kero.

Kwa upande wake mgombea huyo amewahakikishia wananchi kuwa atasimamia changamoto za ukamilishaji wa miradi mbalimbali inayoikabili kata hiyo ikiwemo ujenzi wa Zahanati na ukarabati wa bara bara, kuendeleza ujenzi wa shule ya sekondari ya khiyo kuwa ni ya gharofa na kuandika historia kuwa ni kata ya kwanza jijini Arusha kuwa na shule ya ghorofa.


Amesema changamoto zingine zilizopo katika kata hioyo ni kuongeza vyumba vya madarasa katika shule ya msindi Daraja mbili kutoka 28 ili vitosheleze mahitaji

Kuhusu ukosefu wa ajira amesema hilo ni tatizo la dunia nzima hivyo akaahidi  kuanzisha vikundi vya vijana 25 kila mtaa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kufyatua tofari, kuwatafutia mitaji akina mama kupitia Saccos kutokana na kutokuwa na mitaji na kuwataka waachane na malumbano ya vyama vya kisiasa kwa sababu hayana tija .

.Amesema iwapo atachaguliwa atawahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa itikadi ya kisiasa wala dini kwa sababu  yeye atakuwa ni kiongozi wa wote .

kwa upande wake mstahiki Meya, wa Jiji la Arusha, Gaudensi Lyimo, amewaomba wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea huyo ili aweze kuhudhuria kwenye vikao vya baraza la madiwani ambavyo ndivyo  vyenye maamuzi ndani ya halmashauri na kero zao zitapatiwa ufumbuzi.kwa faida ya wananchi.

 Amesema madiwani waliopita wa Chama kimoja cha siasa wamekuwa hawataki kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani kutokana na maelekezo ya viongozi wao na matokeo yake ni kukwamisha  wananchi jambo ambalo ni tofauti na ahadi zao  na pia linaenda kinyumne na demokrasia.

iwapo watachagua diwani ambae hahudhurii vikao ni nani atawawakilisha kwenye vikao vya baraza la madiwani na kuwasemea kuhusu kero zilizopo

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Ally Nyanya, omar Sheh, amevionya vyama vya kisiasa kutokuthubutu kuchoma bendera za CCM, katika kata hiyo kama vinavyojinasibu, na akawakumbusha kuwa kinachotakiwa ni maendeleo na sio vurugu.

Amesema wakithubuti kuchoma bendera ya CCm, katika kata hiyo kama wanavyojinasibu watambue kuwa mwisho wao umefika atawasaka mmoja mmoja mpaka kieleweke kwa sababu anawafahamu wote .

No comments:

Post a Comment