Thursday, October 11, 2012

JIJI LA ARUSHA LAWATAKA WANAOISHI MABONDENI KUHAMA KWANI MVUA ZITAKUWA NYINGI



Na Queen Lema, ARUSHA

KAIMU mkurugenzi wa manispaa ya Arusha Bw Omary Mkombole amewataka wananchi wa manispaa hiyo ambao wanaishi mabondeni kuhama mara moja ili kuepusha majanga mbalimbali ya mafuriko ambayo yatatokana na mvua kubwa za vuli ambazo ziunatarajiwa kuanza hivi karibuni

Bw Mkombole aliyasema hayo jana wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kupokea taarifa maalumu kutoka mamlaka ya hali  ya  hewa Tanzania (TMA)ambayo ilidai kuwa mkoa wa Arusha utakuwa na mvua nyingi sana

Alisema kuwa kutokana na taarifa hiyo wananchi wanapaswa kuhama wenyewe tena kwa haraka sana hasa wale ambao wanaishi katika maeneo ya mabondeni mwa manispaa ya Arusha kwani endapo  kama watakiuka hayo basi watasababisha sana maafa hasa  nyakati hizo za mvua kubwa

“Taarifa ambayo tumeipokea hapa inasema kuwa ni lazima wananchi wachukue tahadhari mapema sana kwani kutakuwa na ongezeko kubwa sana la mvua zinazortarajiwa kuanza kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa huu na kumalizika mwezi wa kumi na mbili hivyo hii ni amri ya Manispaa kuwa wananchi hao wanatakiwa kuhama mara moja “alisema bw Mkombole

Hataivyo alitaja maeneo ambayo yanaweza kukabiliwa na maafa ya mafurukio hasa nyakati za mvua kubwa ni pamoja na maeneo ambayo yapo kwenye miteremko mikali, kwenye makorongo mbalimbali,ambapo kuanzia sasa wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari ya kuhama maeneo hayo ambayo wataalamu wamedai kuwa yana kabiliwa na hatari sana.

Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kuwa mbali na tahadhari ya mafuriko pia Halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa Mji wa Arusha unakuwa na mpangilio wa hali juu hususani kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa ambapo wanatakiwa kuuza bidhaa zao kwa kufuata sheria mbalimbali za majiji ya Kimataifa duniani

Alisema kuwa kwa sasa Manispaa hiyo itahakikisha kuwa tatizo la uuzwaji wa bidhaa unafuatwa kwa haraka sana ambapo wafanyabishara wote wanatakiwa kuuza bidhaa zao ndani ya maduka yao sanjari na kutumia Mabohari ili kuufanya mji wa Arusha kuwa katika kiwango cha usafi wa hali ya juu sana

“tunachokitaka hapa ni kuwa tuhakikishe kuwa hii hali ambayo ipo ya uuzaji wa vitu holela na makazi ya kiholela ndani ya mji huu inakwisha kabisa ili mji huu uweze kurudi katika hali na hadhi ya kuwa jiji tena la Kimataifa Ulimwenguni lakini kama tutaendelea na uuzaji wa bidhaa ovyo ovyo basi tutachangia sana jiji nalo kuwa ovyo kabisa”aliongeza bw Mkombole

No comments:

Post a Comment