Thursday, October 11, 2012

Mifuko ya jamiii yatakiwa kufanya utafiti kubaini wanachama wapya



Naibu Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akifungua mkutano 22 wa mwaka wanachama wa mfuko wa pensheni wa (PPF)
………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Mifuko ya jamii hapa nchini imetakiwa kufanya utafiti wa kina ili kubaini wanachama wapya kutoka kwenye sekta isiyo rasmi kwani sekta hiyo imekuwa ikikuwa kwa kasi na kuajiri watu wengi hivyo wajikite kutafuta wateja wapya kwenye sekta hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa fedha Mh.Saada Mkuya Salum wakati akifungua mkutano 22 wa mwaka wanachama wa mfuko wa pesheni wa (PPF)na wadau mbali mbali wa mifuko ya hifadhi za jamii kutoka nchi za Sadc.
 
Mh.Mkuya aliwataka PPF na wadau wengine kuisidia serikali kukuza uchumi kwa kuweka misingi endelevu ya uendeshaji wa huduma muhimu za hifadhi ya jamii hapa nc hini katika mazingira haya ya utandawazi na kuwaasa viongozi wa mifuko ya hifadhi za jamii kuhakisha mifuko yao inaongeza mapato yatokanayo na uwekezaji wa miradi mbali mbali sanjari na usajili wa wanachama wapya.
 
Mh.Mkuya pamoja na kuupongeza mfuko wa PPF kwa jitihada zao za kuhakikisha maendeleo ya kweli yanapaitikana hapa nchini zikiwemo ujenzi wa nyumba za bei nafuu pamoja na utoaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo na viwanda na kuwataka kuendelea kuwekeza zaidi hususani katika sekta za maendeleo ya kijamii wanachama wake waendelee kufaidika.
 
“Naomba kutoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta za maendeleo ya kijamii ili wanachama wanufaike na zoezi hilo liende sambamba na mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii kutoa elimu kwa wanachama juu ya vipi wanavyofaidika kutokana na uwekezaji huo”alisema Saada.
 
Aidha mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa PPF Dkt. Adolfu Faustine Mkenda alisema kuwa mfuko wa PPF unaendelea kufanya vizuri kwa thamani ya mifuko kuongezeka kufikia shilingi bilioni 894.52 kutoka shilingi 722.47 bilioni mwishoni mwa mwaka 2010 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 23.8% ambapo hadi kufikia mwezi wa sita mwaka huu thamani ya mfuko iliongezeka na kufikia 984.99 bilioni.
 
Mkenda alisema kuwa idadi ya wanachama imeendelea kuongezeka hadi kufikia wanachama 180,049 mwishoni mwa mwaka 2011 ikilinganishwa na wanachama 160, 068 waliokuwepo mwishoni mwaka 2010 na hadi mwezi juni mwaka huu wanachama wameendelea kuongezeka zaidi na kufikia 195,347.
 
Pia aliongeza kuwa michango ya wanachama iliyokusanywa  kwenye mifuko hadi kufikia mwezi wa sita mwaka huu 111.44 bilion zimekusanywa ambapo lengo lilikuwa ni kukusanya shilingi 108 bilion kwa kipindi cha miezi sita ambayo ni sawa na 103% ya makisio ambapo mfuko umeendelea na uwekezaji katika vitega uchumi na jumla ya shilingi 837 bilioni ziliwekezwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2011 ukilinganisha na mwaka 2010 na hivyo kuvuka lengo la mapato yao.
 
Nae mkurugenzi wa PPF hapa nchini William Erio alisema kuwa shirika linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kubadilika kwa riba katika amana za uwekezaji,kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei, ufinyu wa wigo katika uwekezaji na zingine ni uwasilishwaji wa fomu kutoka kwa waajiri au kutowasilisha, ucheleweshaji wa michango, hivyo shirika limeamua kukabiliana kikamilifu na changamoto hizo ili kuleta tija na mafanikio kwa wanachama wao.

No comments:

Post a Comment