NA ASHURA MOHAMED,ARUSHA
Idadi ya
vifo vinavyotokana na uzazi imepungua
kwa asilimia hamsini ikilinganishwa na mwaka
2009 ambapo takwimu zinaonesha kuwa vifo vilikuwa 500 huku mwaka 2010
vifo vilipungua na kufikia 250 ambapo lengo halisi ni kupunguza vifo vya
akinamama na kufikia 193 ifikapo mwaka 2015.
Akizungumza wakati
wa kufungua mkutano wa Afya ya Mama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.mohamed Gharibu Bilal alisema kuwa serikali inajitahidi
kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa ili kuhakikisha kuwa vifo visivyo vya
lazima havitokei tena.
Dkt.Bilal
alisema kuwa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua ni lazima suluhu ipatikane
ili kuweza kuzuia matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea akinamama hao kupoteza
maisha hivyo kupitia mkutano huo ni wazi kuwa watashirikiana vyema katika
kupeana utaalam kwa nchi zilizofanikiwa ili kuokoa maisha wa wanawake.
Alisema kuwa
baadhi ya nchi ambazo zinashiriki katika mkutano huo wa kimataifa tayari
wameshapiga hatua kubwa hivyo kupitia nchi hizo ni wazi kuwa mafanikio
yatapatikana na hatimaye Tanzania itaweza kufikia malengo kwa kupunguza vifo
vianavyotokana na uzazi.
Aidha amefafafunua
kuwa takwimu zinaonesha kuwa nchi za kiafrika zinazoendelea vifo vya akinamama
ni vingi sana ambapo kwasasa ni asilimia 99 ya akinamama wanapoteza maisha
kutokana na vifo vya uzazi.
“Nataka
naomba niwaelezeni kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na asasi zisizo za
kiserikali ili kuweza kupunguza vifo vya akinamama na kuhakikisha kuwa mama
yeyote hafariki dunia kutokana na uzazi na watoto pia wasipoteze maisha kwa
magonjwa ambayo yanazuilika.”alisema bilal
Kwa upande
wake waziri wa Afya Dkt.Hussein Mwinyi alisema kuwa alisema kuwa wazira yake
kwa kushirikiana na serikali ina mikakti ya kuhakikisha kuwa kila mama anapata
lishe kabla ya kubeba ujauzito ili aweae kuapata nguvu za kujifungua na kuwa na
afya bora.
Alisema kuwa
changamoto nyingine inayopelekea vifo kwa akina mama ni usafiri ambapo akina
mama wengi wanajifungulia njiani kutokana na umbali pindi wanapotafuta huduma
za afya.
Pia kwa sasa
serikali itatoa vifaa vya kujifungulia bure ili akina mama wote waweze
kujifungulia katika vituo vya afya kwa
kuwa nusu ya akinamama wanajifungulia nyumbani kwa uoga wa kulipia gharama za vituo vya afya.
Naye Mkurugenzi
wa asasi ya (MDH) dkt.Chalamila Guerino alisema kuwa mkutano huo utakuja na maazimio ya namna ya kusaidia kupunguza vifo kwa akinamaama kwa
kuboresha huduma ya afya ili wanaweze kufikia malengo ya millennia.
Mwisho……………
No comments:
Post a Comment