WAFADHILI kutoka Ujerumani wamefanikiwa kutoa msaada wa
vitabu venye thamani ya Milioni tisa kwa shule ya sekondari Leguruki iliopo
Wilayani Meru mkoani Arusha kwa lengo la kuongeza ufanisi wa elimu zaidi kwenye
shule hiyo.
Akiongea na wanafunzi shuleni hapo mapema jana mara baada ya
kupokea msaada huo Mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Arusha John Palangyo
alisema kuwa msaada huo utasaidia sana
shule hiyo ya sekondari ambayo pia ipo chini ya Chama cha mapinduzi.
Palangyo alisema kuwa wafadhili hao wameamua kutoa msaada
huo wa vitabu venye thamani ya milioni tisa lakini ni wajibu wa wanafunzi
kuhakikisha kuwa wanavisoma na kuvifanyia kazi vitabu hivyo kwani vina mitaala
ya nchi ya Tanzania
Pia alsiema kuwa kama
wanafaunzi wa shule ya sekondario yoyote ile hapa nchini watakuwa na tabia ya
kujisomea vitabu mbalimbali basi watachangia kwa kiwango kikubwa uelewa tofauti
na sasa ambapo bado wapo wanafunzi wanaosoma kwa kufundishwa na walimu pekee.
Alibainisha kuwa kuna umuhimu mkubwa sana
wa walimu wenyewe kuhakikisha kuwa wanawasisitiza wanafunzi kujisomea vitabu na
kuachana na tabia ya kujidanganya kuwa hata wasiposoma watakuwa na maisha
mazuri tena yenye mvuto wa hali ya juu jambo ambalo nalo linachangia sana kuongeza idadi ya
wanaofeli katika shule za Sekondari pamoja na Vyuo vikuu hapa nchini
“mimi napenda kuwaambia kuwa msije kuona kuwa watu
wana
maisha mazuri mkadhani kuwa hawakujituma kusoma vizuri shuleni ni lazima
kama mnataka maisha mazuri basi mjitume kusoma kwa bidii
lakini pia msikubali kujiwekea fikra ambazo zinawapotosha kwani hizo
ndizo
zinazochangia ninyi mje kuwa na maisha
mabaya hapo baadae”aliongeza Palangyo
Katika hatua nyingine aliwataka hata walimu kuwatengenezea
wanafunzi mazingira mazuri na kuwapa
motisha wanafunzi hasa kwenye suala zima
la usomaji wa vitabu kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuruhusu walio wengi
kupenda kujisomea vitabu.
Awali mkuu wa shule hiyo ya Leguruki Emanuel Loi alisema
kuwa msaada huo wa Vitabu umekuwa na tija kubwa sana shuleni hapo kwani hapo awali shule
nzima ilikuwa na vitabu 52 na sasa wameweza kufanikiwa kupata vitabu zaidi ya
elfu jambo ambalo litaweza kuwanufaisha wanafunzi shuleni hapo
Alimaliiza kwa kusema kuwa hata wazazi nao wana jukumu kubwa
sana la
kuhakikisha shule za sekondari zinakuwa na Vitabu vya kutosha ili kuweza
kuharakisha maendeleo ya elimu
No comments:
Post a Comment