Na Gladness Mushi,Arusha
IDADI ya wabunge wanawake kwenye nchi wanachama wa mabunge ya nchi za
kusini mwa Afrika (SADC) imeongezeka ingawaje kwa Tanzania bado baadhi ya
wanawake wanahofu kubwa ya kushiriki katika chaguzi mbalimbali kutokana na
changamoto zilizopo kwenye jamii
Hayo yameelezwa
na Anna Makinda ambaye ni Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiongea na vyombo vya habari mapema
leo kuhusiana na mkutano wa 34 wa jukwaa
la Mabunge ya Nchi wanachama wa jumuiya
ya maendeleo kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa
Raisi dkt Gharib Bilali mapema jumapili ijayo.
Aidha
Makinda alisema kuwa kuongezeka kwa wabunge wanawake katika mabunge ya SADC
kunatokana na juhudi mablimbali ambazo zinafanywa na jumuiya hiyo hali ambayo
nayo imefanya mabadiliko makubwa sana kwenye baadhi ya nchi.
Alisema kuwa
pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya wabunge wanawake katika jumuiya hiyo
lakini kwa Tanzania bado baadhi ya wanawake wanauoga na hofu ya kushiriki
katika chaguzi kuu jambo ambalo wanatakiwa kulipinga.
"hapa
tunaona kuwa hii idadi ya wanawake ni kubwa katika jumuiya hii ya SADC lakini
kupitia ongezeko hili ni muhimu sana kwa wanawake wa Tanzania nao wakahakikisha
kuwa wanajitokeza kwenye chaguzi mbalimbali na kushiriki kwani uwezo wa wao
kuwa wabunge upo na wasiogoope wala kujiwekea udhaifu wa changamoto”aliongeza
Makinda
Wakati huo
huo alidai kuwa wanawake wa Tanzania hawapaswi kukatishana tamaa wao kwa wao na
badala yake wanatakiwa kupena moyo hasa pale wagombea wanawake wanapokutana na
changamoto kubwa ambazo wakati mwingine zinasababisha baadhi yao kukimbia
nafasi za uongozi
Awali
akiongelea mkutano huo wa 34 alisema kuwa Nchi ya Tanzania imepewa nafasi ya
kuwa mwenyeji mkuu wa mkutano huo ambao utaweza kuwashirikisha viongozi wa Mabunge
mbalimbali kutoka SADC na hivyo kupitia mkutano huo wataweza lkujadili mambo
mbalimbali
Makinda alisema
kuwa mkutano huo utaaangalia vitu muhimu kwa nchi wananchama kama vile vigezo vya kusimamia na kutathimini mwenendo
wa chaguzi za nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
“Kauli mbiu
ya mkutano huu ni vigezo vya kuendesha
na kutathimini chaguzi kwa nchi za kusini
mwa Afrika hivyo basi hapa tutaweza kuangalia na kukagua hilo hivyo
tutaweza kupata hata majibu ambayo yatasaidia nchi zetu”aliongeza Makinda.
MWISHO
No comments:
Post a Comment