Na Queen Lema,Arusha
KUSHINDWA KUFUATILIA MAENDELEO YA WANAFUNZI MASHULENI CHANZO CHA WANAFUNZI KUPEWA ALAMA ZA JUU HUKU WAKIWA HAWANA SIFA ZA KUPATA ALAMA HIZO
IMEELEZWA kuwa kutokana na tabia ya baadhi ya wazazi pamoja
na walezi kushindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni kumesababisha
kukithiri kwa wizi wa mithiani kwenye baadhi ya shule binafsi,huku wanafunzi
wengine wakiwa wanapewa alama za juu wakati hawana uwezo wa kupata alama hizo.
Hayo yameelezwa na Bw
Wilson Shange ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shule ya Sotwa iliopo maeneo ya
Ilboru katika maafali ya tatu ya shule hiyo yaliyofanyika mapema jana.
Bw Shange alisema kuwa zipo baadhi ya shule ambazo msimamo
wake ni kuwapa alama za juu wanafunzi huku wanafunzi hao wakiwa hawana uwezo wa
kupata alama za juu hali ambayo inachangia sana kukithiri kwa wingi wa Mambumbu ingawaje
wazazi wanajisifia kuwa watoto wanasoma
Alisema kuwa mbali na hiyo kuweza kuongeza idadi ya mambumbu
tena wanaolipiwa ada pia inachangia sana hata
kiwango cha elimu ndani ya Nchi ya Tanzania kupungua kwa kiwango
kikubwa ingawaje Serikali inalia na kiwango cha elimu kinachotolewa kwa shule
binafsi.
Alifafanua kuwa hali hiyo inachangiwa sana
na baadhi ya wazazi au walezi ambao wanawapeleka watoto wao shule za binafsi
kwa kuwa baadhi yao
wana mila potofu kuwa mwanafunzi wa shule binafsi hana haja ya kufuatiliwa
maendeleo yake
Bw Shange aliongeza kuwa hali hiyo inasababisha kukithiri
kwa changamoto kubwa sana
ndani ya shule hizo binafsi kwa kuwa baadhi ya shule na walimu ambao hawana
maadili ndio wanapata fursa pekee ya kuanza kufanya udanganyifu wa kuwapa
wanafunzi alama za juu huku wanafunzi hao wakiwa hawana uwezo huo
Aliongeza kuwa endapo kama wazazi na walezi wangekuwa na
tabia ya kufuatiliwa maendeleo ya watoto wao shuleni basi wasingeweza kupewa
alama za juu hivyo wangechangia sana
maendeleo ya wanafunzi tofauti na sasa ambapo baadhi ya wazazi wanashindwa
kufika mashuleni kwa kisingizio kuwa ni shule binafsi.
“inakuwa ni ngumu sana kwa baadhi ya shule hata kufanya
maamuzi ya kitaaluma kwa kuwa wazazi na walezi hawaonekani kabisa wanajua
ukishalipa ada umemaliza mchezo wa elimu kwa kweli tunakabiliwa na changamoto
hiyo na kama wazazi na walezi wataendelea hivi ni wazi elimu ya hapa nchini
itaendelea kushuka badala ya kupanda”aliongeza
Bw shange
Awali aliongeza kuwa ndani ya Shule hiyo ya Sotwa wameweka
msimamo mbalimbali wa kuhakikisha kuwa wanafukuza wanafunzi ambao wazazi wao
hawana mila na desturi za kufuatilia maendeleo ya watoto wao kwani kwa
kuwafukuza watasababisha taaluma kupanda sanjari na maadili ambayo yamepotea sana tofauti na kuaacha
kujua maendeleo ya mwanafunzi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment