IMELEZWA kuwa ukosefu wa huduma za uhakika za maji hasa
maeneo ya vijijini ni chanzo mojawapo cha ongezeko la mimba za utotoni lakini pia uvunjikaji wa ndoa
nyingi huku hali hizo zikisababisha pia ongezeko la watoto mitaani ndani ya mji
wa Arusha
Pia hali hiyo ya ukosefu wa maji kwenye kaya pia
inasababisha umaskini wa hali ya juu sana
ingawaje Serikali kwa sasa inaweka mikakati mbalimbali ya kupambana nao.
Hayo yameelezwa na Bi Asha Shabani ambaye ni Katibu wa Mradi
wa maji ujulikanao kama Mangole uliopo maeneo
ya Kisongo jijini hapa,wakati akielezea mradi huo lakini pia umuhimu wa miradi
ya uhakika ya maji hasa kwa maeneo ambayo yapo nje ya miji
Asha alisema kuwa ukosefu wa maji ya uhakika hasa katika
maeno ambayo yapo nje kidogo ya miji ni changamoto kubwa sana kwa wanawake kwa kuwa asilimia kubwa
huambulia uchovu lakini pia hata kipigo kutoka kwa wenza wao kwa kuwa hutumia muda
mrefu kwa ajili ya kusaka maji
Mbali na hayo alisema kuwa ukosefu huo hauathiri pekee
wanawake bali hata mabinti wadogo ambao baadhi ya vijana hutumia mwanya huo
katika kuwadanganya ili waweze kuwapa maji au kuwasaidia kubeba maji kwa uraisi
jambo ambalo nalo ni chanzo kikubwa cha mimba za utotoni lakini pia mdondoko wa
elimu kwa watoto wa kike
Akiongelea Mradi huo wa MANGOLE ambao unawasaidia wananchi
kutoka katika kata za Matevesi,Ngorobobu, na Lemguru alisema kuwa umekuwa ni
faida kubwa sana kwenye jamii hiyo kwani hapo
awali kulikuwa na matatizio mengi sana
Alitaja matatizo hayo ni pamoja na baadhi ya wanawake kukosa
ndoa,huku wengine wakiambulia wajukuukabla ya wakati kutokana na udanganyifu
ambao ulikuwa uanendelea kwa watoto wa kike na vijana pia.
“hapo awali tulikuwa tunalazimika kwenda kilomita mpaka 20
kwa siku ili kutafuta maji lakini toka mradi huu uletwe kwa hisani ya Word
Vision umekuwa na faida kubwa sana na hivyo tunataka tuhakikishe kuwa hata
wanawake wa maeneo mengine ndani ya mkoa wa Arusha nao wanaweza kufaidika na
miradi kama hii ili waweze kuepukana na changamoto za uhaba wa maji”aliongeza
Asha
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Mradi huo ambaye ni Profesa
Calvin Marealle alisema kuwa pamoja na kuwa mradi huo umekuwa ni faida kubwa
sana kwa jamii lakini bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile Ukosefu
wa umeme wa uhakika hali ambayo wakati mwingine inasababisha baadhi ya wananchi
kutoka katika vijiji hivyo vitatu kukosa maji ya uhakika
Profesa Marealle aliongeza changamoto nyingine ni pamouja na
baadhi ya wananchi kuiba na kuharibu miundombinu ya maji hali ambayo ni chanzo
kikubwa sana
cha hasara kwenye miradi hiyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment