VIONGOZI wa
makampuni ya ulinzi mkoani arusha
yametakiwa kutoa taarifa za mafunzo yanayoendana na kazi zao kwa jeshi la
polisi ili kuwawezesha wafanyakazi wao kupatiwa mafunzo ya kuongeza ujuzi wa kufanya kazi wawapo katika malindo yao.
Hayo yalisemwa
na mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani hapa bi Mary Lugola alipokuwa akifungua kongamano la chama cha wafanyakazi walinzi(TUPSE) na wadau wa ulinzi binafsi lililofanyiika mjini hapa.
Bi Mary
alisema kuwa kwa sasa jeshi la polisi liko tayari kutoa mafunzo yanayoendana na
kazi zao kwa makampuni mbali mbali
hivyo viongozi wa makampuni hayo yahakikishe
kuwa yamezingatia vigezo ili kuwawezesha
wafanyakazi hao kunufaika na mafunzo hayo.
Aidha aliwataka askari kuwa na nidhamu na
kuhakikisha kuwa huduma wanazozitoa kwa wananchi ni nzuri sio za kejeli kwa
kuwa wapo baadhi ya askari ambao sio waaminifu wawapo katika kazi zao.
Kwa upande
wake katibu wa chama cha wafanyakazi walinzi
kit aifa bw Godiwin Mariki alisema kuwa
katika chama chao kumekuwepo na changamoto lukuki ikiwemo ya
wateja kulazimisha rushwa ya fedha kutoka kwa waajiri walipotoa tenda ya
ulinzi na pale waajiri wanapokuwa
hawatoi rushwa hizo basi wateja hao huvunja lindo na kuwapatia waajiri wengine.
Alisema kuwa
kupitia jambo hili wanaiomba serikali ikemee vitendo hivyo na kuagiza malindo
yatolewe kwa mkataba isiyopungua mika mitatu ili kuwezesha waajiri kuwa na
uwezo wa kuwahudumia walinzi wake.
Pia alitaja
changamoto ingine kuwa ni pamoja na
wanawake kuachishwa kazi pale wanapopata ujauzito na kutolipwa mishahara wakati
wakiwa likizo ya uzazi kwa madai kuwa ni starehe yao na haimhusu mwajiri, hivyo
kuitaka serikali kukemea na kuchukua hatua kwa kuwa huo ni uonevu.
Aidha TUPSE
imependekeza kuwa sera na sheria ya ulinzi binafsi iharakishwe ili kuondokana
na maonezi mengi yanayofanyiwa walinzi ,waajiri,wateja na jamii inayowazunguka
.
Mwisho..
chanzo cha habari na Queen Lema,
ARUSHA
No comments:
Post a Comment