WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WAKUSUDIA KUNUNUA KIWANDA CHA CHAI KATUMBA
habari na francis godwin
Wakulima wakichuma chai yao
Timu ya wanahabari kutoka mkoa wa Iringa na Dar
WAKATA
wakulima wadogo wa chai wilayani Mufindi na Njombe wakiendelea
kulia na unyanyasaji wanaoupata kutoka kwa makampuni makubwa ya chai
kwa kununua chai yao chini ya kiwango ,chama cha wakulima wadogo
wa chai wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanatarajia kununua kiwanda cha
wakulima Tea Compani (Katumba ) ili waweze kukimiliki kama njia ya
kuepukana na manyanyaso ya makampuni dhidi ya wakulima wa zao hilo
imefahamika.
Wakulima
hao wadogo wa chai Rungwe wamefikia hatu hiyo kama njia ya
kuepukana na manyanyaso ambayo wameendelea kuyapata ikiwa ni pamoja na
kuuza chai yao kwa bei ya chini zaidi .
Akizungumza
na timu ya wanahabari mwenyekiti wa chama hicho cha wakulima
wadogo wa chai Rungwe Johnson Mwakasege alisema kuwa pamoja na
changamoto mbali mbali ambazo wakulima wa chai wamekuwa wakizipata
ila kwa upande wa wakulima wa chai Rungwe wameendelea kunufaika
zaidi na kilimo cha chai kupitia msaada mkubwa wanaoupata kutoka
taasisi ya utafiti wa chai Tanzania (TRIT) kwa hisani ya jumuiya ya
Ulaya (EU) hivyo wamepanga kuepuka manyanyaso hayo na hivyo
kukusudia kununua kiwanda cha chai Katumba ili waweze kumiliki
wenyewe.
Alisema
kuwa kwa sasa wakulima hao wa chai wadogo wanamiliki kiwanda hicho
kwa hisa alisimilia 30 na asilimia 70 inamilikiwa namwekezaji huku
mipango yao kwa mwakani kuweza kumiliki hisa zote 100 katika
kiwanda hicho.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa kiwanda hicho cha katumba wanakusudia kununua
kwa shilingi bilioni 2.6 na tayari mazungumzo yameanza na ikiwezekana
mwakani 2013 wakulima hao wataanza kuendesha kiwanda hicho.
Kwani
alisema kuwa lengo la wakulima wa chai Rungwe ni kuweza kuwawezesha
wakulima kuwa na sauti kubwa katika kiwanda hicho na kuweza
kuongeza malipo ya chai kutoka shilingi 206 ambazo wanalipwa sasa na
kufikia bei nzuri zaidi itatayomwamasisha mkulima kuweza kupanua
mashamba zaidi ya chai .
Hata
hivyo alisema kuwa chama hicho cha wakulima wadogo wa chai
Rungwe kwa sasa kina mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kutoka
kiasi cha shilingi milioni 10 ambazo wakulima hao walikuwa nazo mwaka
1998 walipo anza umoja huo .
Mwakasege
alisema kuwa mbali ya kukusudia kununua kiwanda hicho bado
wakulima hao wadogo wameweza kujenga ofisi yao ya kisasa kwa kiasi
cha shilingi milioni 500 kama njia ya kujiimarisha zaidi .
Aidha
alisema kuwa chama hicho cha wakulima wa chai Rungwe kimetenga
kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI
wilayani humo ili kupunguza vifo vya vijana vinavyotokana na ugonjwa
wa UKIMWI na kupelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa na kuwaacha wazee
wakiendelea kubeba mzigo mkubwa wa kuhudumia mashamba ya chai .
MWISHO
No comments:
Post a Comment