KIKUNDI CHA OLGILAI CHANGAMKENI YOUTH GROUP CHAFANIKIWA
KUTOA MSAADA WA MADAWATI,NA VIFAA VYA SHULE YA OLGILAI
Na Queen Lema, Arusha
KIKUNDI cha Olgilai Changamkeni Youth Group kilichopo maeneo
ya Olgilai mkoani Arusha kwa kushirikiana na wadau wengine wa elimu wameweza
kutoa msaada wa madawati zaidi ya 50 pamoja na vifaa vingine kama vile meza,
kabati, na viti kwa shule ya msingi
Olgilai huku lengo likiwa ni punguza changamoto za kielimu shuleni hapo
Hataivyo msaada huo ambao ulitolewa mapema jana ulienda
sanjari na uzinduzi wa kikundi hicho ambacho kimelenga kutatua changamoto mbalimbali
katika kijiji hicho cha Olgilai na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Akiongea mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule ya
msingo Olgilai Mwenyekiti wa kikundi hicho Benjamini Justin alisema kuwa
wameamua kuchangia zoezi zima la elimu ili kwenda sanjari na mpango wa serikali
wa matokeo ya haraka(BRN)
Benjamini alidai kuwa hapo awali shule hiyo ilikuwa
inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya ukosefu
wa madawati na vifaa vingine hali ambayo ilifanya wazazi wa eneo hilo ambao ni wanakikundi
kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Alifafanua kuwa baada ya kuweka mikakati mbalimbali waliweza
kuwashirikisha wadau wengine ambao nao waliweza kuungamkono na kuhakikisha kuwa
wanapunguza tatizo la uhaba wa madawati kwenye shule hiyo ya Olgilai.
Wakati huo huo alidai kuwa pamoja na kuwa wameweza
kufanikisha kutoa msaada huo wa madawati, meza,viti, madaftari, na kalamu
lakini bado wanakabiliwa na changamoto lukuki ambazo wakati mwingine
zinakwamisha jitiada zao
Alitaja changamoto hiyo kuwa ni pamoja na baadhi ya fursa za
mikopo ni finyu kwa kuwa taasisi hizo hazitoi mikopo kwa vikundi jambo ambalo
linakwamisha jitiada za maendeleo ya vikundi hasa vile vya mitaa.
“pamoja na kuwa leo tumeweza kutoa msaada huu kwa shule hii
pamoja na kuzindua rasmi kikundi chetu bado changamoto hii tunaifikiria sana hivyo basi tunaomba taasisi za Fedha kuhakikisha kuwa
zinatuangalia ili nasi tuweze kusaidia jamii kama
tulivyofanya leo”aliongeza Benjamini
Wakati huo huo akiongea kwa niaba ya wanafunzi ambao ndio
walengwa wa msaada huo Irene Peter alidai kuwa msaada huo wa madawati utasaidia
sana kuongeza
ufanisi wa elimu kwani hapo awali wanafunzi shuleni hapo walikuwa wanalazimika
kuandika Miandiko mibaya kwa kuwa hawakuwa na madawati.
No comments:
Post a Comment