Na Queen Lema,Arusha
WAMILIKI WA SHULE BINAFSI WATAKIWA KUWAANGALIA YATIMA NA
WALE WANAOTOKEA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
IMEELEZWA kuwa endapo kama Wamkiliki wa shule binafsi wataweza kusaidia jamii za watoto yatima na
wanaotokea katika mazingira magumu katika shule zao basi watachangia kwa
kiwango kikubwa sana
kupunguza tatizo la watoto wa mitaani.
Asilimia kubwa ya watoto wanaokimbilia mitaani wanakwena
huko kwa kuwa baadhi ya familia zao hazina uwezo wa kuwasaidia katika masuala
ya elimu hali ambayo nayo kwa wakati mwingine inasababisha wimbi la watoto hao.
Kauli hiyo imetolewa na
Bi Isabela Daniel ambaye ni Mkurugenzi wa Shule ya Upendo Friends iliopo
Matevesi Jijini hapa mapema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
waliotembelea shule hiyo kwa malengo ya kutambua nafasi ya Watoto Yatima ndani
ya shule Binafsi.
Isabela alisema kuwa kwa sasa kutokana na hali ya Maisha sio
wanafunzi wote ambao wana uwezo wa kwenda shule hasa za binafsi na hata zile za
Serikali hivyo basi kama wamiliki wa shule watakuwa wanaaacha kuliangalia suala
hilo kwa undani ongezeko la watoto wa mitaani litakuwa ni kubwa sana.
Alifafanua kuwa wamiliki wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa
kuhakikisha kuwa kila mara wanaweka utaratibu wa kuwachukua japo kidogo na kuwapa elimu wanafunzi ambao wanatokea katika
makundi maalumu japo kwa uchache ambapo pia hali hiyo itachangia sana nafasi ya maendeleo katika taifa la Tanzania.
Awali Mkurugenzi huyo alisema kuwa nayo Serikali kwa
kushirikiana na Shule Binafsi zinatakiwa kuhakikisha kuwa zinaweka utaratibu wa
kutambua vipaji vya baadhi ya watoto kwani kwa sasa wapo baadhi ya watoto ambao
wanavipaji lakini wanashindwa kuendelezwa
Alisema kuwa hali hiyo ya kuendeleza vipaji vya watoto
itafanya baadhi yao waweze kujiimarisha zaidi
hivyo hata kwa nyakati zijazo pia watachangia sana
kupunguza tatizo la wataalamu ambalo kwa sasa linaikabili sana
Nchi ya Tanzania.
MWISHO
No comments:
Post a Comment