Na Queen Lema, Arusha
CHUO cha Uasibu Arusha kimefanikiwa kuongeza
mapato yake kutoka kiasi cha Milioni 200 hadi kufikia milioni 900 kwa
kila mwaka kutokana na kuongeza fani mbalimbali za masomo hasa katika Shahada
za Uzamili ya Uongozi na
Biashara katika Teknolojia ya Habari, Shahada ya Uzamili ya Uongozi na Biashara
katika Ugavi pamoja na Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Fedha na Uwekezaji
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa chuo hicho
Profesa Johanes Monyo katika maafali ya tatu ya chuo hicho yaliyofanyika Mapema
jana Mjini hapa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali
Aidha Profesa huyo alisema kuwa hapo awali
mapato ya Chuo hicho yalikuwa yapo chini lakini mara baada ya kuongeza fani
mbalimbali za elimu wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Milioni 900 jambo ambalo
limeweza kuwapa wadau mbalimbali wa Chuo hicho kuweza kutafuta Njia nyingine ya
kuweza kuongeza fani mbalimbali huku fursa hizo nazo zikiwanufaisha watanzania
walio wengi zaidi
“Hili ongezeko la fedha limetokana na fani hizi ambazo
tunazitoa hapa lakini tunashirikiana na chuo kimoja cha uingereza ambacho
kinajulikana kama Coventry cha Uingereza
na kwa kweli tumeona matunda makubwa sana kwa kuwa wanafunzi waliopata elimu
hii mbali na kuajiriwa katika sekta mbalimbali pia wataweza kujiajiri wao
wenyewe na kuweza kushindana na soko la ajira hapa Afrika mashariki na duniani
kote’aliongeza profesa Johanes.
Hataivyo
alisema kuwa kutokana na ongezeko hilo chuo
hicho bado kina mkakati wa hali ya juu sana
wa kuhakikisha kuwa kinabuni mbinu mbadala za kuweza kuongeza mapato sanjari na
kuhakikisha kuwa nao watanzania wananufaika hata kwakushirikiana na vyuo vya
nje ya Nchi.
Katika hatua
nyingine alisema kuwa nao wahitimu wa vyuo mbalimbali wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanajiwekea utaratibu wa kusoma kwa malengo ya kujiajiri toafuti na pale
ambapo kwa sasa asilimia kubwa ya wasomi wanashindwa kufikia malengo yao kwa kuwa wanasoma kwa
ndoto za kuajiriwa
Alifafanua
kuwa endapo kama wasomi ambao ni vijana wa Taifa la Tanzania
watasoma kwa ndoto za kujiajiri basi wataweza kuchangia sana
hata kufanya mabadiliko ya hali ya juu sana
katika soko la Ajira ambalo baadhi ya vijana wanashindwa kulipata kwa kuwa wana
ndoto za kuajiriwa tena Serikalini.
“kama mhitimu
wa chuo chochote kile leo ataweza kujiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa
anasoma kwa malengo ya kujiajiri yeye mwenyewe basi ataongeza juhudi zaidi
kuliko kusubiri kupewa ajira ambazo kwa sasa ni ndogo sana kwa kuwa kuna wimbi
kubwa sana la wahitimu kutoka katika vyuo mbalimbali hapa nchini’aliongeza
Profesa Johanes.
Kwa upande wa
wahitimu ambao walikuwa 127 walisema kuwa bado kuna uitaji wa wataalamu katika
nyanja mbalimbali hasa kwa nchi ya Tanzania hivyo Serikali inatakiwa
kuendelea kuwekeza zaidi katika vyuo ili kuweza kufikia malengo mbalimbali ya
Milenia.
MWISHO
No comments:
Post a Comment