Tuesday, January 15, 2013

WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI KWA KUSHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUANZA RASMI MKAKATI WA KUJENGA HOSTELI SHULE ZOTE






WILAYA YA ARUSHA VIJIJINI KWA KUSHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUANZA RASMI MKAKATI WA KUJENGA HOSTELI SHULE ZOTE

Na Queen Lema,ARUSHA


Wilaya ya Arusha vijijini kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi,inatarajia kufanya mabadiliko katika sekta ya elimu ambapo kwa sasa wanatarajia kujenga na kuimarisha hosteli kwa ajili ya wanafunzi hususani watoto wa kike ambao wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta elimu huku wakiwa mbioni kupatwa na Vishawishi mbalimbali.

Endapo kama tutajenga hosteli za kutosha basi hata kiwango cha elimu yetu nacho kitaweza kupanda kwa hali ya juu sana tofauti na sasa ambapo wanafunzi wanalazimika kupanga nyumba”GETO”ili wasome karibu na shule.

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Arumeru Magharibi ambaye pia ni Naibu waziri wa ardhi Goodlucky  ole Medeye wakati akikabidhi hundi kwa halmashauri ya Arusha vijijini  ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Olokii  mapema wiki hii.

Medeye alisema kuwa ameamua kuwa balozi wa hosteli kwenye shule za Jimbo lake kwa kuwa bado watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto nyingi sana hasa  ya kutembea umbali  mrefu huku wengine wakipanga nyumba hali ambayo inawafanya washindwe kusoma kwa raha huku hali hiyo nayo ikichangia sana washindwe kufanya vema katika masomo yao.

Alisistiza kuwa lengo lake halisi ni kuona kuwa hosteli zinakuwa ni nyingi sana ambapo wanafunzi watakaa mashuleni na kisha kusoma kwa raha huku pia hosteli hizo nazo zikichangia sana waweze kuondokana na Vishawishi ambavyo wanakutana navyo wakati wakiwa njia kuja au kurudi  majumbani  mwao

“Vishawishi kwa mtoto wa kike ni vingi sana lakini  kama sote tutainuka na kuhaikisha kuwa hawa tunakuwa na hosteli za kutosha basi itaweza kuraisisha sana maendeleo ya elimu lakini kama tutakuwa na tabia ya kujivunia eti wingi wa shule wakati watoto wanatembea umbali mrefu kutafuta elimu na barabarani wanakutana na vishawishi kibao ni wazi kuwa bado tutakuwa hatujafanya chochote kipya kabisa”aliongeza Medeye

Katika hatua nyingine alisema kuwa ili lengo hilo la ujenzi wa hosteli liweze kukamilika tena kwa wakati katika baadhi ya shule ndani ya Jimbo na Halmashauri yake ni lazima kuwepo na Ushirikiano tena wa hali ya juu sana ili kuweza kuwanusuru  watoto kutoka katika nyumba za kupangisha”GETO”

MWISHO.

No comments:

Post a Comment