Tuesday, January 15, 2013

VIONGOZI WA NJANJA MBALIMBALI TANZANIA WATAKIWA KUACHA MAOVU ILI KUOKOA TAIFA DHIDI YA LAANA MBALIMBALI


VIONGOZI WA NJANJA MBALIMBALI TANZANIA WATAKIWA KUACHA MAOVU ILI KUOKOA TAIFA DHIDI YA LAANA MBALIMBALI

IMEELEZWA kuwa kutokana na tabia ya baadhi ya Viongozi wa Serikali kujihusisha na utafutaji wa mali ambazo si halali,Rushwa,pamoja na ukatili kumesababisha Umaskini pamoja na Laana kubwa sana kwa baadhi ya watanzania

Asilimia kubwa ya viongozi wan chi katika nyanja tofautitofauti ambao wanajihusisha na masuala hayo kumechangia sana madhara makubwa na hata wengine kufanya wananchi ambao wanawaongoza kufanya matendo ambayo ni ya kikatili na machafu mbele za mungu.

Hayo yamebainishwa na Mchungaji Wilson Laizer wa kanisa la T A G Christian Centre lilopo Enaboishu mkoani hapa wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo wiki iliyopita.

Mchungaji Laizer alisema kuwa Viongozi wa Nchi ambao wanatafuta mali na mafanikio kwa njia ambazo si halali kunachangia sana madhara makubwa sana kwa nchi hivyo viongozi hao sasa wanatamkiwa kuhakikisha kuwa wanamgeukia Kwanza Mungu kabla ya kuvisha Nchi laana ya mafaniko ambayo si ya halali.

Alisema kuwa Viongozi wa nchi ambao tayari wamejihusisha na halin kama hiyo wanatakiwa kwanza kuhakikisha kuwa wanatubu na kujutia ambacho wamekifanya ambapo hali hiyo itaweza kuruhusu Roho ya toba hata kwa wale ambo wamewazulumu kwa njia moja au nyingine katika utafutaji wa mali

“kutafuta mali kwa nguvu huku ukitumia mbinu ambazo zinamkandamiza mwenzako si jambo zuri sana bali ni jambo ambalo linafanya Nchi kuwa na machafuko na mambo ambayo si mazuri ni vizuri hata viongozi wetu wa sasa wakajua kuwa kumzulumu mtu mali yake na hata haki zake ni vibaya sana hivyo nawasihi sana ninyi ndugu zangu mhakikishe kuwa mnaomba toba hata kwa watu wengine ili muweze kuokoa nchi ya Tanzania “alisema Mchungaji huyo

Awali alisema kuwa hata kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa wabinifu tena wa hali ya juu sana hasa katika kumtafuta na kujaribu kuuteka ufalme wa Mungu  ili waweze kufikia malengo yao ya kiroho na hata ya kimwili.

Alibainisha kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kuepukana na tabia ya kuwekezewa zaidi fikra na Utukufu wa shetani ambao mara zote ni utukufu wa uongo na badala yake wataweza kuliongoza taifa kwenye mpango wa Mungu ambao unahitajika tena kwa haraka sana kuendelea kutumika ndani ya Nchi ya Tanzania.

MWISHO

No comments:

Post a Comment