Wednesday, January 30, 2013

WATOTO WA KIKE WAKIPEWA MOYO NA MOTISHA WANA UWEZO WA KUSHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA MITHIANI YA KITAIFA





WATOTO WA KIKE WAKIPEWA MOYO NA MOTISHA WANA UWEZO WA KUSHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA MITHIANI YA KITAIFA

,Arusha

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya watoto wa kike wanashindwa kufanya vema katika mithiani ya mwisho pamoja na masomo ya Sayansi kwa kuwa wanakatishwa tamaa na jamii zao hasa walimu na wazazi

Watoto wa kike wana uwezo mkubwa sana wa kufanya vema na kushika nafasi za juu katika masomo na mithiani yao lakini kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya kukatishwa tamaa hali ambayo inawafanya washuke Kitaaluma

Hayo yameelezwa na Mwanafunzi bora  katika  Mthiani wa darasa la saba  mkoa wa Arusha, na Wilaya ya Arusha Vijijini,Pricilla Calvin Marealle wakati akiongea na Majira mapema jana kuhusu kiwango cha Ufaulu wa watoto wa kike kwa mkoa wa Arusha

Alisema kuwa watoto wa kike wana uwezo mkubwa sana wa kufanya vema katika mithiani yao ya Mwisho na hivyo kushika nafasi ya juu Kitaifa endapo kama mfumo ambao upo katika baadhi ya familia na Shule utabadilika

Akielelezea mfumo huo ambao unasababisha wanafunzi wa kike kushindwa kufanya vema ni pamoja na kukatishwa tamaa hasa katika masomo ya Sayansi na hivyo wanafunzi wa kike kuishia kuambiwa kuwa masomo ya Sayansi ni masomo ya wanafunzi wa Kike hali ambayo nayo inachangia sana wanafunzi kubweteka sana

Aliongeza kuwa mfumo mwingine mbaya ambao unasababisha kwa kiwango cha juu sana wanafunzi wa kike kushindwa kufanya vema katika masomo yao ni pamoja na wazazi, na walimu kukaa mbali na wanafunzi wao na hivyo kushindwa kuwapa moyo wa kufaulu huku wazazi wakiona jukumu hilo ni kwa ajili ya walimu na walimu wakiona kuwa jukumu hilo ni kwa ajili ya wazazi hali ambayo inawafanya watoto wa kike kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea

“Mimi naweza kusema kuwa nimekuwa mtoto wa pili Kimkoa na wa Kwanza kimkoa kwa kuwa walimu wangu na wazazi na ndugu zangu walikuwa wanafuatilia maendeleo yangu tangu nilipokuwa madarasa ya awali na pale nilipoanguka walitafuta chanzo  na kunipa moyo na motisha mbalimbali ndio maana niliweza kufika hapa na hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kujifunza juu ya suala hili kama wanataka wanafunzi waweze kufaulu”alisema Pricilla

Awali alitoa wito kwa Serikali nayo kuhakikisha kuwa wanaboresha zaidi shule za Kata hasa upande wa Maabara ambapo kwa sasa napo kuna changamoto Lukuki ndani ya shule hizo hali ambayo inafanya hata wakati mwingine wanafunzi wa shule za Kata kuonekana kama ni watoto wa maskini kutokana na uhaba wa vifaa vya kujifunzia.

MWISHO

No comments:

Post a Comment