Wednesday, January 30, 2013

TANZANIA INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO



TANZANIA INAKABILIWA NA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO

TANZANIA inakabaliwa na tatizo la uhaba wa  mafundi Sanifu Maabara ambapo kwa sasa wanaozalishwa na Vyuo vya Ufundi hapa nchini hasa Arusha Techical College(ATC)ni ndogo sana hali ambayo inafanya baadhi ya shule za Sekondari hapa nchini kukosa ufanisi zaidi na Masomo ya Sayansi

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa elimu na Ufundi hapa Nchini Bw Philiph Mulugo wakati akiongea na wadau mbalimbali wa chuo cha ufundi Arusha(ATC)mapema wiki hii

Aidha Mulugo alisema kuwa bado hali si shwari hasa katika sekta hiyo ya mafundi sanifu wa maabara kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye shule za Sekondari zaidi ya 400 wakati wanaozalishwa wakiwa bado ni 15

Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kuwepo na uhitaji mkubwa sana wa mafundi sanifu kwa kuwa ili shule yoyote ile iweze kufanya vema katika masomo ya Sayansi ni lazima kwanza wataalamu hao waweze kuandaa vifaa mbalimbali vya maabara ili kuruhusu wanafunzi wasome vizuri

“hapa unaweza kuona kuwa wahitimu  wa hii fani wachache sana kuliko wahitimu wa darasa la saba ambao wanatarajia sasa rasmi kuanza rasmi masomo ya Sayansi sasa kwa hali hii hata wale walimu wa masomo haya kwa kweli wanazidiwa sana na majukumu lakini kama watakuwa na wataalamu wa kutosha tunaamini kabisa  ufaulu wa masomo haya utaongezeka sana hivyo Serikali itaondokana  hata na uhaba wa wataalamu mbalimbali”aliongeza Mulugo

Mulugo pia alisema kuwa pamoja na uhaba huo wa mafundi sanifu wa maabara lakini lengo la Serikali la sasa ni kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na  Wataalamu hao ambao wataweza kushirikiana na walimu wa Sayansi hivi karibuni ambapo pia hata Vyuo vya ufundi navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kuzalisha wataalamu wengi zaidi

Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuhakikisha kuwa kamwe hawakimbii fani hiyo badala yake wajiunge na Chuo hicho cha  Ufundi Arusha ili waweze kudahiliwa kama wataalamu  ambapo hali hiyo itaweza kuokoa Jamii ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu hao

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Richard Masika alisema kuwa kwa sasa Jamii inaona Masomo ya Sayansi ni Magumu kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuyafundisha kwa vitendo jambo ambalo kwa sasa chuo hicho kimejipanga sana kuweza kujipanga kudahili wahitimu wengi zaidi ili kufanya masomo hayo yasionekane ni magumu

Dkt Masika alisema kuwa ili masomo hayo yasionekane kuwa ni magumu kwa sasa wamejiopanga kwa kuhakikisha kuwa wanazalisha wataalamu wengi zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 watakuwa wamezalisha wataalamu zaidi ya 150 ambao wataweza kusaidia sana kuokoa shule zenye uhaba wa watalaamu hao

MWISHO

No comments:

Post a Comment