Friday, January 25, 2013

MBUNGE LEMA AMTUNISHIA MISULI MKUU WA WILAYA,AFUNGA SHULE,MKUU WA WILAYA AIFUNGUA KWA GHAZABU KUBWA

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA JOHN MONGELA AKIFAFANUA JAMBO ARUSHA,PICHA NA MAKTABA YA MALKIA WA MATUKIO




Na  Queen Lema,Arusha

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela ameshukia Mbunge wa Jimbo la Arusha  mjini, Goodbless Lema  mara baada ya mbunge huyo kuifungia shule ya Sekondari Korona mapema  jana na kudai kuwa mbunge huyon hana mamlaka ya kufunga shule na asitumie kofia ya ubunge kuvunja Sheria na kuharibu amani ya Jiji la Arusha

Hatua hiyo imekuja leo mara baada ya Mbunge huyo kufungia shule ya sekondari Korona kwa madai kuwa shule hiyo bado changamoto nyingi sana  na hivyo wanafunzi wanasoma masaa mawili mpaka matatu hivyo ni bora kila mwanafunzi ahamishwe na kwenda shule nyingine


Akiongea katika mkutano uliohitishwa na uongozi wa jiji la Arusha Mkuu wa Wilaya,alisema kuwa,kitendo cha Mbunge Lema kufunga shule sio kitendo cha  kuvumiliwa kwa kuwa yeye ndiye mtungaji wa Sheria lakini yeye pia ndiye mvunjaji mkubwa sana wa Sheria hivyo pamoja na kuwa amefunga shule na kuwataka wanafunzi kuondoka ndani ya shule hiyo bado hajawasaidia wanafunzi hao,kwa kuwa jumatatu asubui watarudi na kuendelea na masomo

Alifafanua kuwa endapo kama Mbunge Lema angeona kuwa shule hiyo ya Korona ina matatizo ambayo ameyataja basi angeyatatua kwa kuwa shule hiyo bado ipo ndani ya jimbo na pia ipo ndani ya eneo ambalo anaishi hivyo bado anakuwa chanzo cha kudididimiza maendeleo ya shule hiyo

“haiwezekani mtu akalale na mke wake nyumbani alafu kesho aibuke aseme kuwa shule ya kata haina vigezo kama tutavumilia hili suala la Lema basi kesho na diwani naye atafunga shule kwa kuwa haina vigezo na  viwango  sasa mimi kama mkuu wa wilaya nasema kuwa hili suala halitavumilika ingawaje pia baadhi ya madai ya Lema ni kweli ila kabla ya yote angetakiwa aaangalie sheria ya mwaka 1995 inavyosema juu ya ufungaji wa shule”aliongeza Mongela

Awali Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa madai ambayo Lema ameyatoa ni ya kweli na pia anaungana nae ingawaje anachomlaumu ni kushindwa kushirikiana na Viongozi ili Viongozi wazembe waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Nchi

Mongela alisema kuwa suala la ukosefu wa Maji,Vyoo, na Usafi sio suala la hiari la kutekelezwa na Viongozi wa jiji bali ni suala la lazima kutekelezwa ingawaje mpaka sasa changamoto kama hizo hazijatatuliwa kwenye shule hiyo,na badala yake viongozi wa Jiji wamekaa ndani ya Ofisi zao ilihali wanafunzi wanateseka sana

“Leo tunasema kuwa Lema amefunga shule lakini tuangalie ukweli wa madai yake yupo sawa na mtanisamehe wakati mwingine mimi nitamuunga mkono na kumsaidia katika mambo yake kwa kuwa  wapo baadhi ya watendaji wabovu  ndani ya Halmashauri mnashushia hadhi Serikali na kwa hili mtaondoka mmoja baada ya mwingine na ninaanza na Mkuu wa Shule hii”alisema Mongela

“huyu mkuu wa shule ambaye ni John Ndewila amekuwa ni chanzo kikubwa sana cha haya matatizo ambayo yamepelekea leo shule kutangaziwa kufungwa sasa kwa hali hiyo nasema kuwa naanza nae kwa kumshusha cheo kuanzia sasa ni mwalimu wa kawaida na mpaka jioni barua imfikie’aliongeza Mongela

Awali aliongeza kuwa wanafunzi wa shule hiyo wanatakiwa kurudi shuleni hapo siku ya jumatatu na kuachana na kauli ya Mbunge kuwa shule imefungwa lakini pamoja na hayo Jiji la Arusha kwa kushirikiana na Mkurugenzi,na Afisa elimu sekondari wanatakiwa kuweka maji ndani ya siku moja pamoja na kutatua changamoto  za shule hiyo lakini kama hawatafanya hivyo watavuliwa madaraka

Katika hatua nyingine Lema alisema kuwa kamwe Mkuu wa Wilaya hapaswi kumuingilia katika majukumu yake kwa kuwa yeye amechaguliwa na wananchi wakati Mkuu wa Wilaya ameteuliwa na Raisi

Lema alisema kuwa anachokitafuta machoni mwa watu na Mungu ni haki na wala sio sifa kwa kuwa alipofunga shule hiyo alikuwa na viongozi wa Serikali,kama Vile Afisa elimu Sekondari,Afisa utumishi  na kwa hali hiyo ni vema kama Jiji likasaidia  na kutatua changamoto ambazo zimo kwenye shule za Kata.

MWISHO


No comments:

Post a Comment