Tuesday, January 15, 2013

LIPIENI MILIONI MBILI ZA ALAT TUTATUE CHANGAMOTO AMBAZO ZIPO KWENYE JAMII ZENU KWA PAMOJA





LIPIENI MILIONI MBILI ZA ALAT TUTATUE CHANGAMOTO AMBAZO ZIPO KWENYE JAMII ZENU KWA PAMOJA

Na Mwandishi wetu,ARUSHA

HALMASHAURI  za mkoa wa Arusha zimeagizwa kutoa kiasi cha Milioni mbili kama mchango kwenye Jumuiya ya Serikali za mitaa kwa mkoa wa Arusha(ALAT)ambapo michango hiyo itaweza kusadia na kutatua changamoto mbalimbali hasa kwenye Serikali za Mitaa

Agizo hilo limetolewa Mapema wiki hii na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Goodson Majola wakati akiongea na wananchama wa umoja huo mjini hapa

Majola alisema kuwa ni vizuri kwa kila Halmashauri kuhakikisha kuwa inachanga kiasi hicho na kuachana na tabia ya kukwepa michango mbalimbalin kwani kwa kutotoa Michango ndani ya Umoja huo unachangia sana maendeleo kuwa hafifu sana

Alisema kuwa Michango hiyo ina umuhimu mkubwa sana hususani kwa wakati kama huu ambao  jamii inakabiliwa na matatizo makubwa ambayo yanaitaji ufunguzi tena kuanzia ngazi za Serikali za mitaa.

“ni lazima kila halmashauri iweze kutoa na kuchangia kiasi cha Milioni mbili kuanzia sasa na Halmashauri ambayo haitachangia kiasi hicho kwa wakati kwa kweli hautaweza kuwatambua kwani chombo hiki kina nafasi kubwa sana ya kuweza kutatua matatizo ya wananchi hivyo Umoja ni muhimu sana na tutumie chombo hiki katika kutatua kero za wananchi’aliongeza Majola.

Katika hatua nyingine wadau wa Umoja huo walisema kuwa pamoja na kuwa Halmashauri zinatakiwa kuachana na Tabia ya kukwepa Michango mblimbali lakini Jumuiya hiyo inapswa kuhakikisha kuwa inatatua kero ambazo zipo kwenye Serikali za mitaa hasa Migogoro ya ardhi na Mipaka.

Akiongea suala hilo Diwani wa Mwandeti,Boniface Tarakwa alisema kuwa sehemu pekee ya kupata muafaka wa masuala ya migogoro ni kwenye ALAT kwa kuwa ina meno ya kuweza kutoa  majibu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali hali ambayo itachangia sana Amani.

Tarakwa aliongeza kuwa matatizo ya Migogoro ya Ardhi imesababisha madhara makubwa sana na inatakiwa kumalizwa tena kwa haraka kupitia kwenye umoja huo hasa kwa kuyafikisha kwenye sehemu muafaka hasa kwenye vikao vikuu vya mkoa.

“Jambo la msingi hapa ni jumuiya hii ihakikishe kuwa inamulika hata shida ambazo zipo na itusemehee kwenye ngazi za juu kwani zipo baadhi ya ngazi ambazo zinatupiga chenga  na huku kwenye jamii tunaonekana kama wasanii hivyo Matumizi mazuri ya jumuiya hii yatachangia sana maendeleo na nafasi nzuri kwenye jamii ambayo tunaiongoza’aliongeza Tarakwa.

MWISHO

No comments:

Post a Comment