Wednesday, January 30, 2013

CCM MERU WATAKELEZA AHADI ZA CHADEMA




CCM MERU WATAKELEZA AHADI ZA CHADEMA

Na Queen Lema,Meru

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi  Wilaya ya Meru(CCM) kimetekeleza ahadi iliyotolewa na Viongozi wa Kitaifa wa chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kupitia kwa Mbunge wa jimbo hilo Joshua Nassari, ambapo viongozi hao walitoa ahadi ya kuchimba Visima 11ndani ya siku 90 katika Kata ya Maroroni kijiji cha Samaria lakini ahadi haijatekelezwa

Akiongea na Vyombo vya habari mapema jana Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Meru,Furaini Mungure alisema kuwa Viongozi wa Chadema ambao ni Dkt Slaa,Ndesamburo, na Mbowe walitoa ahadi hizo wakati walipochukua jimbo la Meru Mashariki lakini hawakutekeleza ahadi hiyo ambayo ikuwa inadai kuwa watapeleka na kwenda kuchimba Visima 11 katika eneo Samaria Wilayani Meru

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo Ccm imeona kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hiyo ambayo walikuwa wameahidiwa wananchi lakini bado haijatekelezwa hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana  kutokana na ukame uliokithiri ndani ya maeneo hayo

Alifafanua kuwa pamoja na kuwa Viongozi hao wa Chadema wametoa ahadi hiyo ya uchimbaji wa Visima lakini Ccm imeweza kufanikisha na kutekeleza ilani yake ambayo inasema na kudai kutekeleza mahitaji mbalimbali ya wananchi ambayo  kama hayatatekelezwa chanzo chake ni umaskini uliokithiri sana

“ahadi ilitolewa na Chadema na ilikuwa itekelezwe ndani ya siku 90 mara baada ya Mbunge wao kupewa madaraka na wanananchi haikutekelezwa lakini Sisi Ccm Tumetekeleza tena kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo shida kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ilikuwa ni uhaba wa maji sasa sisi kwa kushririkiana na Halmashauri ya Meru  tumeweza kumaliza mchakato huo visima “aliongeza

Akielezea Utekelezaji wa Ahadi hiyo ya Visima 11 ambayo ilitolewa na Chadema alisema kuwa Ccm tayari imeshakamilisha mchakato wa kupeleka maji katika kijiji cha Samaria, ambapo mpaka kufikia mwezi wa tatu wananchi hao watapata maji

Mungure alibainisha kuwa Chama chake kitajenga Tanki la maji lenye ujazo wa lita elfu hamsini ambapo wananchi hao wataweza kupata maji kwa uraisi sana tofauti na sasa ambapo wanalazimika kutembea Umbali mrefu sana kutafuta maji

Mbali na hayo alisema kuwa  nao viongozi wa Ccm hawatakiwi kukaa maofisini na badala yake wanatakiwa kwenda kwenye jamii na kuangalia jinsi ya kutatua changamoto ambazo zinaikabili ili kuweza kutekeleza ilani ya Chama hicho.

MWISHO

No comments:

Post a Comment