Tuesday, January 15, 2013

LEMA ATETA NA MAFISADI WANAOTUMIA MAKANISA NA MISIKITI KWA AJILI YA KUJISAFISHIA

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GOODBLESS LEMA AKIHUTUBIA WANANCHI KATIKA MOJA YA MIKUTANO YA HADHARA




LEMA ATETA NA MAFISADI WANAOTUMIA MAKANISA NA MISIKITI KWA AJILI YA KUJISAFISHIA

Na Queen Lema,ARUSHA


MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema ameyataka makanisa na Misikiti hapa nchini kuachana na tabia ya kuwakumbatia mafisadi kutokana na wingi wa sadaka zao na badala yake kuwaombea mafisadi hao waweze kubadilika

Asilimia kubwa ya mafisadi bila kujali imani zao sasa wanatumia sana Makanisa na Misikiti ili kwenda kujisafisha kwenye jamii kwa kuchangia kiwango kikubwa sana cha fedha huku fedha hizo za sadaka zikiwa ni  fedha chafu

Lema aliyasema hayo Jijini hapa wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake mapema jana,huku lengo halisi likiwa ni kukumbuka siku ya January tano ambayo baadhi ya wananchama wa Chadema walipoteza Maisha

Aidha Lema alisema kuwa tabia hiyo ambayo kwa sasa imeibuliwa na mafisadi ya kujisafisha kupitia vyombo vya dini si tabia njema kabisa bali ni tabia ambayo inapeleka nchi na kizazi chake mahala pabaya sana huku pia hali hiyo ikichangia Umaskini mkubwa sana kwenye jamii ya watanzania

Alisema kuwa wananchi kamwe hawapaswi kukubaliana na hali hiyo ya mafisadi sasa kutumia majumba ya ibada na kujisafisha bali na wao wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi ili waepukane na fedha chafu ambazo zinatolewa na mafisadi kwenye majumba ya ibada kama harambee

‘mimi nashangaa sana ninyi viongozi wa majumba ya ibada ambao kila kukicha mnakaa na kuomba Rehema lakini Mafisadi wakija na Fedha chafu hamuwaulizi na badala yake ndio mnawawekea mikono ya baraka sasa hamuwezi kuona kuwa mnawawekea mikono waendelee na kazi yao ya kuwaibia wananchi wa Tanzania?alisema Lema

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa yeye ni Mbunge lakini kamwe hatukubali kuona kuwa anahujumiwa ili awaache wananchi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa wananchi hao ndio waliomuamini na wakampa kura ili aweze kuwaongoza tena kwa njia ya uhalali kabisa

Alisisitiza kwa wananchi kuwa ipo haja ya watu wote kumrudia zaidi Mungu na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa mwaminiufu kwani uaminifu pekee ndio utakaoleta maendeleo ya Mkoa wa Arusha pamoja na Nchi ya Tanzania tofauti na kutegemea fedha chafu za harambee kutoka kwa Mafisadi

Hataivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Arusha(CHADEMA)kiliweza kutoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya watoto yatima huku lengo likiwa ni kukumbuka mauji dhidi ya wanachama wa chama hicho yaliyofanyika January 5 mwaka jana.

MWISHO

No comments:

Post a Comment