Tuesday, January 15, 2013

MAKAMU WA RAISI ADAI KUWA VIFO VYA UZAZI VIMEPUNGUA KWA ASILIMIA 50

DKT GHARIB BILALI AKISISTIZA JAMBO LEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO,AICC,PICHA NA ASHURA MOHAMED

NA ASHURA MOHAMED,ARUSHA


Idadi ya vifo  vinavyotokana na uzazi imepungua kwa asilimia hamsini ikilinganishwa na mwaka  2009 ambapo takwimu zinaonesha kuwa vifo vilikuwa 500 huku mwaka 2010 vifo vilipungua na kufikia 250 ambapo lengo halisi ni kupunguza vifo vya akinamama na kufikia 193 ifikapo mwaka 2015.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Afya ya Mama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.mohamed Gharibu Bilal alisema kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa ili kuhakikisha kuwa vifo visivyo vya lazima havitokei tena.

Dkt.Bilal alisema kuwa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua ni lazima suluhu ipatikane ili kuweza kuzuia matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea akinamama hao kupoteza maisha hivyo kupitia mkutano huo ni wazi kuwa watashirikiana vyema katika kupeana utaalam kwa nchi zilizofanikiwa ili kuokoa maisha wa wanawake.

Alisema kuwa baadhi ya nchi ambazo zinashiriki katika mkutano huo wa kimataifa tayari wameshapiga hatua kubwa hivyo kupitia nchi hizo ni wazi kuwa mafanikio yatapatikana na hatimaye Tanzania itaweza kufikia malengo kwa kupunguza vifo vianavyotokana na uzazi.

Aidha amefafafunua kuwa takwimu zinaonesha kuwa nchi za kiafrika zinazoendelea vifo vya akinamama ni vingi sana ambapo kwasasa ni asilimia 99 ya akinamama wanapoteza maisha kutokana na vifo vya uzazi.

“Nataka naomba niwaelezeni kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali ili kuweza kupunguza vifo vya akinamama na kuhakikisha kuwa mama yeyote hafariki dunia kutokana na uzazi na watoto pia wasipoteze maisha kwa magonjwa ambayo yanazuilika.”alisema bilal

Kwa upande wake waziri wa Afya Dkt.Hussein Mwinyi alisema kuwa alisema kuwa wazira yake kwa kushirikiana na serikali ina mikakti ya kuhakikisha kuwa kila mama anapata lishe kabla ya kubeba ujauzito ili aweae kuapata nguvu za kujifungua na kuwa na afya bora.

Alisema kuwa changamoto nyingine inayopelekea vifo kwa akina mama ni usafiri ambapo akina mama wengi wanajifungulia njiani kutokana na umbali pindi wanapotafuta huduma za afya.
Pia kwa sasa serikali itatoa vifaa vya kujifungulia bure ili akina mama wote waweze kujifungulia katika vituo vya  afya kwa kuwa nusu ya akinamama wanajifungulia nyumbani kwa uoga wa  kulipia gharama za vituo vya afya.

Naye Mkurugenzi wa asasi ya (MDH) dkt.Chalamila Guerino alisema kuwa mkutano huo utakuja  na maazimio ya namna  ya kusaidia kupunguza vifo kwa akinamaama kwa kuboresha huduma ya afya ili wanaweze kufikia malengo ya millennia.

Mwisho……………

No comments:

Post a Comment