Saturday, January 12, 2013

MBUNGE AMSHUKIA MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUHUSU MIGOGORO YA MIPAKA





Mbunge wa Jimbo la Longido Lekule Laizer amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kuhakikisha kuwa anatatua tena kwa haraka migogoro ya kimipaka baina ya Wilaya na Wilaya kwani Migogoro hiyo imekuwa ikichangia Umaskini mkubwa sana

Lekule aliyasema hayo wiki hii katika kikao cha Maendeleo ya Mkoa wa Arusha (RCC) wakati akichangia hoja ya migogoro baina ya wilaya yake na Wilaya za Arusha vijijini, pamoja na Monduli

Lekule alisema kuwa kwa sasa ni aibu kubwa sana kuona Serikali ipo madarakani lakini suala zima la Migigogoro bado lishika nafasi kubwa sana kwenye jamii hasa za wafugaji na wafugaji  hali ambayo nayo inaongeza umaskini mkubwa sana kwenye jamii hizo

Aliongeza kuwa Kamwe atakayeweza kutatua Migogoro hiyo ni Mkuu wa Mkoa ambapo yeye kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali watatumia elimu zao katika kusulihisha jambo ambalo mpaka sasa bado halijapatiwa ufumbuzi tena wa Kutosha


“inanisikitisha sana kuona kuwa Mkuu wa Mkoa yupo lakini bado migogoro ya ardhi ndio inashika kasi kubwa ndani ya jamii sasa tuende wapi jamani na mbona hili ni jambo dogo sana  kwa mkuu wa Mkoa tunaomba sasa uamke na uje kuangalia suala hli la  Migogoro kwa kweli linatuchosha sana”alisema Lekule

Aliongeza kuwa kitu kikubwa sana ambacho kitaweza kuepusha Wilaya za Arusha Vijijini,Monduli, na Longido katika migogoro ya mipaka ni kuweka mipaka ambayo itaweza  kuwaonesha wananchi ukomo wao baina ya sehemu moja na sehemu nyingine hali ambayo nayo itaweza kurudisha amani na Umaskini ambao umekithiri sana kwenye jamii

“Kwa nini Mkoa unashindwa kuweka mipaka baina ya Wilaya na Wilaya na ni kitu kidogo sana ambacho hakiitaji Taaaluma kubwa sana sasa kwa kuwa hakuna mipaka wananchi wengi sana wanapigana kila mmoja akidai mwenzake kaingilia sehemu ya mwingine je tunalinda amani au tunabomoa amani ya Nchi jamani ni lazima Mkoa lazima uangalie hili suala la migogoro ya mipaka”alisema Lekule

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo,alisema ,kuwa kamwe viongozi hawapaswi kuja juu kuhusiana na suala hilo la Migogoro ya Mipaka bali wanatakiwa kukuaa na wananchi pamoja na wataalamu ili kutafuta suluhu ya amani ambayo imepotea

Mulongo alisema kuwa suala hilo la Migogoro ya mipaka watahakikisha kuwa wanalishugulikia tena kwa haraka sana lakini pia ili liweze kufanikiwa kwa haraka sana ni lazima juhudi viongozi mbalimbali wa Wilaya ziwepo ili kuondoa Tatizo hilo.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment