KATA ZA MBUGUNI NA MARORONI WILAYANI MERU ZIMEATHIRIWA
VIBAYA NA MABADILIKO TABIA NCHI
Na Queen Lema,MERU
IMEELEZWA kuwa Kata za Mbuguni na Maroroni katika wilaya ya
Meru mkoani hapa imeathirika vibaya sana kutoka
na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kufanya shuguli mbalimbali za kilimo na
mifugo kukwama kwa muda mrefu sana
Hayo yalielezwa na afisa mifugo wa wilaya hiyo Bw Mohamed
Hassan wakati akiongea katika mdahalo wa mazingira hususani tabia nchi
uliondaliwa na mtandao wa asasi binafsi mkoani hapa (ANGONET)mapema jana
Bw Mohamed alisema kuwa kata hizo ambazo zipo kusini mwa
wilaya hiyo ni moja ya kata ambazo zimeonekana kuwa na madhara makubwa sana ya tabia Nchi
kutokana na sababu mbalimbali hali ambayo hata kwa upande mwingine imesababisha
Ukame
Alisema kuwa kitu kikubwa ambacho kimesababisha maeneo hayo
ya kusini mwa wilaya hiyo kukumbwa na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ni
pamoja na mabonde pamoja na Mafuruko ambayo yanahamisha hata rutuba ya udongo
tofauti na maeneo mengine ndani ya Wilaya ya Meru
Aliongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikizaa matunda mabaya sana ya ukame ambapo baadhi ya mazao yameshindwa kustawi
huku baadhi ya mazao kama vile mihogo na Mtama yakistawi kwa shida hivyo
kuruhusu umaskini mkubwa sana
kwa kata hizo ambazo ni tegemezi ndani ya mkoa wa Arusha.
“kwa kweli hapa Meru hii hali imetuathiri sana kwa kuwa hapo
awali haya maeneo yalikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuzalisha lakini sasa
hawawezi kuzalisha kwa wakati hivyo ukame na umaskini ndio umekithiri sana
ingawaje sisi kama sisi tuna mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa tunaokoa
haya maeneo ambayo yameathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi”alisema
Awali mratibu wa mtandao wa asasi binafsi mkoani hapa Bw
Peter Bayo alisema kuwa kuna ulazima mkubwa sana wa kuhakikisha kwanza jamii inakuwa
na uwelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa mabadiliko ya
tabia nchi pamoja na na uharibifu wa mazingira yanachangia sana kudidimiza
uchumi wa nchi na
atajamii
Bw Bayo alisema kuwa endapo kama jamii itakuwa na uelewawa
mambo hayo itakuwa ni raisi sana kuweza kuchukua
tahadhari mapema sana hasa wananchi wa Vijijini
tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya wananchi hawana elimu ya vyanzo vya
mabadiliko hayo hali ambayo inachangia sana
madhara ndani ya jamii.
Mbali na hayo aliwataka nao watandeji wa Serikali
kuhakikisha kuwa wanajiwekea utaratibu wa kuwa na midahalo ambayo itawahusisha
wananchi na hapo wataweza kujadili masuala mbalimbali yahusiyo mabadiliko hayo
tofauti na pale ambapo wananchi wanapopata fursa pindi wanapokutana na asasi
binafsi
MWISHO
No comments:
Post a Comment