Monday, December 3, 2012

FPCT KUJENGA SHULE ZA AWALI,SEKONDARI,NA VYUO VIKUU KWENYE MIJI MIKUBWA NA MAKAO MAKUU YA MIKOA


Na Bety Alex,ARUSHA

FPCT KUJENGA SHULE ZA AWALI,SEKONDARI,NA VYUO VIKUU KWENYE MIJI MIKUBWA NA MAKAO MAKUU YA MIKOA

Kanisa la Free pentekoste church Tanzania(FPCT)limeweka mikakati mbalimbali ya kujenga shule za kuanzia ngazi za shule za awali,sekondari hadi vyuo vikuu kwenye Makao makuu ya mikoa na Miji Mikubwa hapa Nchini huku lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa  waumini wa kanisa hilo pamoja na wananchi wanapata elimu kwa uraisi sana.

Hayo yameelezwa wiki iliyopita na Askofu mkuu wa kanisa hilo Davidi Batenzi katika uzinduzi wa kanisa la FPCT mahali lilopo katika eneo la Napoko Maji ya chai wilayani Meru Mkoani Arusha

Askofu huyo alisema kuwa lengo halisi la kuhakikisha kuwa kila Mji mkubwa na Makao makuu ya makanisa yao yanakuwa na njia ya mbalimbali za kuweza kusadia jamii kwani asilimia kubwa ya wanajamiin bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali hasa ya uhaba wa shule

Alisema kuwa mpango huo ambao kwa sasa umeshaweza kutekelezwa pia utaweza kuisadia Seriakali kwani bado jamii nyingi sana zina huitaji mkubwa sana wa elimu kwani elimu ndiyo msingi imara wa kuepukana na  Umaskini

‘tumejipanga kuhakikisha kuwa ndani ya miji mikubwa tunajenga shule na hata ikiwezekana vyuo vikuu na hii itasaidia sana kuweza kuruhusu waumini wetu kupata elimu kwani elimu nayo ni muhimu sana na kama haya malengo yataweza kutumikan ipasavyo basi itachangia sana elimu ya Tanzania kuweza kukua na kuenda sanjari na nchi ambazo zinazoendelea”aliongeza Askofu huyo.

Awali mchungaji kiongozi wa kanisa hilo FPCT Mahali,mchungaji Japhet Kitomari alisema kuwa uzinduzi wa kanisa hilo umefanikiwa kutokana na mshikamano wa waumini wa kanisa hilo pamoja na waumini wengine ambao nao walichangia kiasi cha Milioni 10.

Mchungaji Kitomari aliongeza kuwa fedha hizo Milioni 10 zimesaidia sana kuweza kuboresha kanisa hilo ambapo pia hata Ofisi ya kanisa hilo nayo imemalizika hali ambayo itaweza kurahisisha kazi ya huduma kwa uraisi tofauti na pale ambapo wanapokuwa hawana ofisi ya kanisa.

‘hizi milioni 10  zilichangwa na waumini wa kanisa hili na waumini wengine na kwa kweli wamefanya kitu kizuri sana na hili jambo litaweza kurahisisha sana kazi za injili ambapo pia hata hapa pia tuna mikakati mingine hata ya kuhakikisha huduma za msingi kama vile shule ambapo ndani ya eneo hili kuna huitaji mkubwa sana’alisema Mchungaji kitomari.

Katika hatua nyingine alisema ili kuweza kujenga na kusaidia jamii hasa ile ya karibu na kanisa hilo la Mahali,alisema kuwa wamejenga shule ambayo itaweza kuwapa fursa watoto wa jirani kusoma kwa uraisi sana

Mchungaji huyo alisema kuwa kupitia shule ambayo ipo chini ya kanisa hilo la Mahali wanafunzi zaidi ya 60 wanasoma kwa gharama ndogo sana(ENGLISH MEDIUM) ambapo kupitia elimu hiyo wataweza kujifunza mambo mbalimbali tena ya kiroho zaidi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment