HASARA NYINGI ZA WAKRISTO ZINATOKANA NA UBAGUZI WA HUDUMA ZA
KANISA
Na Mwandishi wetu. Arusha
Wakristo wanakabiliwa na changamoto ya ubaguzi wa ibada hali
ambayo wakati mwingine ndiyo chanzo cha wao kwenda makanisani kwa mazoea bila
kufanikiwa katika maisha yao huku wengine wakiwa
wnaaambulia hasara za mali
na hali zao kila siku
Asilimia kubwa ya wakristo wana ubaguzi wa huduma za ibada kama vile Maombi,utoaji wa mafungu ya kumi,harambee za
kila siku na michango ya hiari hali ambayo ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya
kanisa.
Hayo yameelezwa na Mchungaji Steven Laizer wa kanisa la Bethel Kishore lilopo maeneo ya Kishore Ngaramtoni jijini
Arusha mapema wiki iliyopita.
Mchungaji Steven alidai kuwa tabia hyo imekuwa na kustawi sana kwenye baadhi ya
maksanisa huku baadhi ya wakristo wakiona kuwa makanisa hayo pamoja na
wachungaji hawawombei kwa kutosha bila kujua na kutambua kinachowafanya
wasiweze kusonga mbele ni uchoyo na ukaataaji wa huduma mbalimbali ndani ya
makanisa.
Alisema kuwa wengi wanajidanganya kuwa huduma ambazo
zinaweza kuwakomboa kwenye maisaha yao
ni huduma za kusifu na kuabudu pekee jambo ambalo sio la kweli kwani huduma
zote Mungu yupo pamoja na wanadamu
“ndani ya kanisa ukiita huduma ya kusifu na kuabudu watuw
ataalikana lakini ita huduma ya maombi hata ya kufunga na kuomba uone kama utaona watu wengi watu wanashindwa kujua na
kutamvbua kuwa ubaguzi wa huduma ndani ya makanisa haufai kabisa na badala yake
unaddiimiza maslahi ya kanisa’aliongeza Mchungaji huyo
Wakati huo huo aliseama kuwa ndani ya makanisa wapo baadhi
ya watu ambao wanaona shida kutoa sadaka kwa madai kuwa hakuna anayewaona na
kisha kuingia mitini jambo ambalo ndilo chanzo cha hasara kwenye maisah yao
“chunguza sana mtu
anayeshidwa kutoa sadaka kwa mungu maisaha yaklle yakoje utakuta kila siku
analia mara ugonjwa, mara hasara, mara wizi sasa kama utakuwa unatoa sadaka ni
wazi kuwa utakuwa unajilinda dhidi ya vitu kama
hivi ambavyo vinacheza kwenye malango ya shetani’aliongeza mchungaji huyo.
Alimalizia kwa kuwataka hata Viongozi wa dini nao
wahakikishe kuwa kamwe hawaoni aibu kuhubiri juu ya vitu mbalimbali ambavyo
vinaweza kuwatenganisha wakristo na huduma za Mungu kwa kuhofia jambo Fulani
kwenye maisha ya kibinadamu ya kila siku.
MWISHO
No comments:
Post a Comment