-WENYEVITI WA VIJIJI VITANO MERU WAMFUKUZA DIWANI MERUWAMPA SIKU 14 KAMA HATAJIUZULU WAO WATAJIUZULU UCHAGUZI
URUDIWE UPYA
-KISA WADAI KUWA DIWANI HUYO NI MCHOCHEZI NA ANALIPIZA
KISASI KWA KUWA HAWAKUMPA KURA 2010
KATIKA hali isiyokuwa
ya kawaida Wenyeviti wa Vijiji Vitano kutoka katika kata ya Nkoaranga Wilayani
Meru mkoani hapa wamemtaka diwani wa kata hiyo kujiuzulu ndani ya siku 14 na
endapo kama hawatafanya hivyo basi wao watalazimika kuachia ngazi kwa kuwa
wanaonewa sana
na diwani huyo
Wenyeviti hao walitoa tamko hilo jana mara baada ya diwani huyo kushindwa
kuwasikiliza kero zao pamoja na za
wananchi na badala yake kupewa maneno ya kashfa yakiwemo maneno ya uvaaji wa
kimaskini huku pia kila siku kuna kithiri wimbi la migogoro
Wakiongea jana na “MALKIA WA MATUKIO”wilayani humo wenyeviti hao
walisema kuwa wanazo sababu maalumu za kumakataa diani huyo ambaye ni Bw
Goodfey Kishongo kwa kuwa yeye ndio chanzo pekee cha vurugu na Migogoro ndani
ya kata hiyo ya Nkoaranga hali ambayo
imesababisha maendeleo kuwa duni sana
Wenyeviti hao ambao wanatokea katika Vijiji Vitano vya Kata
hiyo ambavyo ni Njani, Nshupu,Nkoaranga,Nkoanekoli,na Sangananu walisema kuwa
na endapo kama ataendelea kukaa madarakani
hata kama amepitishwa na wananchi basi baada ya siku 14 wao watajiuzulu
na kupisha uchaguzi mwingine uanze upya kwani hawapati msaada wala ushirikiano
wowote kutoka kwa diwani huyo na badala yake wanaambulia kasfa ya kuitwa
maskini
Walisema kuwa zipo sababu maalumu ambazo zinasabababisha wao
watamke hayo ingawaje wote ni chama Kimoja (CCM) kwani diwani huyo amekuwa
akiwageuka mara kwa mara na hivyo kusisitiza hata migogoro ndani ya jamii huku
pia akishirikiana na Vyama vya Upinzani ili waweze kutoka madarakani na kuachia
wapinzani badala ya CCM
Wakielezea kisa
halisi cha kuwafanyia hivyo ilihali wao wote ni viongozi wa Serikali ya Kijiji
walisema kuwa chanzo halisi diwani huyo anasema kuwa hawakumpa kura kwa mwaka
2010 za udiwani hali ambayo inafanya kila ambaye anamuhisi hakutoa kura anamuharibia kwa wananchi tena
kwa kuwagombanisha na kisha kuibua migogoro ambayo haina ukweli ndani yake .
Waliongeza kuwa mbali na kuwachukia viongozi hao wa Vijiji
kama Vitano vya Kata hiyo ilihali wameshapatanishwa kama mara tatu lakini pia
diwani huyo amelkuwa na tabia ya kugomea miradi mbalimbali ya maendeleo ndani
ya Kata hiyo hali ambayo nayo inachangia
sana Umaskini
kwa vijiji hivyo.
Wakitaja baadhi ya Miradi ambayo diwani huyo amemwaga Sumu
na kusababisha madhara makubwa kwa jamii
ni Pamoja na Mradi wa mbuzi wa
maziwa kutoka katika kijiji cha Nshupu ambao ulitolewa na TASAF ambapo mradi
huo ulitekelezwa na kikundi kimoja lakini bado diwani huyo aliukata na hivyo
kusababisha madhara makubwa kwa wakazi
wa eneo hilo.
Walisema kuwa mbali na eneo hilo la Nshupu lakini pia kwa
maeneo kama vile Nkoaranga alisababisha
mwenyekiti wa Kijiji kufungiwa Nje ya Ofisi na wananchi wenye hasira
kali lakini baadaye ofisi ilifunguliwa chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri,huku
kwa Kijiji cha Sangananu aliwashawishi wananchi kukata zahanati ambayo
ilijengwa na wahisani,na kwa upande wa Kijiji cha Nkoanekoli napo aligomea
vyanzo mbalimbali vya maji hali ambayo ilizua tafrani kubwa sana
Na katika Kijiji cha Njani napo Mgogoro mkubwa sana kwa sasa ni matumizi ya maji ya kuchimba kwa kutumia
mashine ambapo kuna mvutano mkubwa sana
lakini hali hiyo imesababisha baadhi ya kazi za kijamii nazo kusimama kwa kuwa
hakuna umoja madhubuti.
Awali wenyeviti hao kutoka katika Vijiji vitano ambao
wanatarajia kujiuzu endapo kama diwani huyo atajiuzulu ndani ya siku 14 ni
pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkoaranga bw Solomon Sarakikya,Mwenyekiti
kijiji cha Njani bw Elishilia Ayo,mwenyekiti wa kijiji cha Sangananu Bw Sangito
Mafie,na Mwenyekiti wa kijiji cha Nkoanekoli Bw Christopher Pallangyo
Katika hatua nyingine akiongea na “MALKIA WA MATUKIO”kwa njia ya simu
diwani huyo anayetuhumiwa Bw Goodfrey Kishongo alisema kuwa yeye anachokijua ni
kuwa wenyeviti hao wamejiunga na kuwa kitu kimoja kwa kuwa wote wana mapungufu
tena makubwa sana hasa ya ulaji wa mali
za kijiji
Bw Kishongo alisema kuwa bado haogopi kwa kauli ya wenyevit
hao kwa kuwa wao si wananchi na wananchi ndio waliomchagua na kumpa kura hivyo kama wananchi watamkataa ndio ataweza kujiuzulu lakini
kamwe hawezi kujiuzulu kisa wenyeviti wa
vijiji
“bado hawa wenyeviti hawajaongea jambo la msingi mimi ni
,muwazi tena ni mkweli huwa sina mambo ya kupindapinda kamwe wajue kuwa suala la kuachia ngazi sio
suala la matisho kama wanavyofikiri bali ni suala la wananchi wananchi wakisema
hawananitaki hata sasa hivi naacha udiwani”alisema Bw Kishongo
No comments:
Post a Comment