SIDO ARUSHA YAFANIKIWA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA MILION
544,KWA WAJASIMALI 2018
Na Queen Lema,Arusha
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo vidogo hapa
nchini(SIDO)mkoa wa Arusha limefanikiwa kutoa elimu ya ujasiamali kwa
wajasiamali 2,018 huku jumla ya Milioni 544 nayo ikitolewa kama
Mkopo ili kuendeleza mitaji ya wajasiriamali hao kwa kipindi cha miaka miwili,
Hayo yameelezwa na Meneja wa shirika hilo
mkoani hapa Bw Isidore Kayenzi wakati akielezea mafanikio ya Shirika hilo kwa Waziri wa Viwanda
na Biashara hapa nchini Bw Abdalah kigoda mapema jana
Bw Isidore alisema kuwa Mikopo na elimu hiyo ambayo ilikuwa
inatolewa kwa wajasiamali hao imefanikiwa kuwafikia wananchi wa Wilaya za
Arumeru,Monduli,Karatu, longido, na Ngorongoro ambapo mpaka sasa mafanikio yameshaonekana
Aliongeza kuwa mafunzo ambayo wameweza kuwapa wajasiamali
hao ni pamoja na Ujasiamali hasa katika Uongozi wa Kibiashara,utengenezaji wa
sabuni,usindikajiwa ngozi na bidhaa za ngozi,usindikaji wa chakula na matunda,pamoja na mafunzo mengine ambayo
yameweza kutoa ajira huku yakichochea msukumo mkubwa wa Ujasiamali hasa kwa
mkoa wa Arusha
‘hawa wajasiamali ambao tumewapa mafunzo asilimia 70
wameweza kutoa ajira hata kwa watu wengine nah ii imeongeza hata idadi ya viwanda vidogo vidogo ambavyo tunavyo kwa
mkoa wa Arusha ingawaje Sido kama Sido bado inakabiliwa na changamoto za hali
ya juu san”aliongeza Bw Isidore.
Pia alisema kuwa kwa sasa changamoto kubwa sana ambayo
inayokabili Shirika hilo pamoja na wajasiamali wa Mkoa wa Arusha ni Mahitaji makubwa
sana ya wajasiamali wadogo na wakati hasa Mitaji kuliko uwezo ambao wanao hali
ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa undani sana
Alifafanua kuwa mbali na changamoto hiyo ya Ukubwa wa
mahitaji wakati hakuna Mitaji ya kuendeshea shuguli za kijasiamali lakini pia
bado kuna changamoto ya utoaji wa mkopo hasa kwa SIDO kwani kiwango chao cha
juu cha utoaji wa Mikopo ni Milioni sita huku kiwango hicho nacho kikifanya
baadhi ya wajasiamali washindwe kuvuka malengo yao ambayo wamejiwekea hasa ya
kutoa katika daraja dogo na kuingia kwenye daraja la kati la ujasimali.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara hapa Nchini Abdallah
Kigoda alisema kuwa pamoja na kuwa Shirika hilo linakabiliwa na changamoto
mbalimbali lakini bado Tanzania ina tatizo kubwa sana la kutowapa wajasiamali
wadogo na wakati fursa mbalimbali za kukuza na kuimarisha Uchumi wa Mkoa na
Tanzania
Bw Kigoda alisema kuwa kwanza Sekta za umma na binafsi
zinatakiwa kuanza kuwapa fursa wajasiamali wadogo na wakati vipaumbele
mbalimbali kwa kuwa wajasiamali wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kuimarisha hata uchumi ambao
unayumbayumba huku ajira mbalimbali nazo zitaweza kuongezeka.
‘Hii ni Sekta ambayo inatakiwa kupewa kipaumbele kikubwa
sana kwa kuwa ndiyo injayoshikilia mambo mbalimbali na pia nguvu za Ziada zinatakiwa
kuelekezwa kwa wajasiamali wengi zaidi ingawaje hata uwepo wa viwanda vingi
hapa Nchini unachangia sana kuweza kufanya watanzania kupata bidhaa zao kwa
uraisi sana tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya watanzania wanategemea
zaidi bidhaa kutoka nje ya nchi wakati watanzania wana uwezo wa kutengeneza
bidhaa hizo”aliongeza Bw Kigoda.
No comments:
Post a Comment