Na Queen Lema, Arusha
SERIKALI imefanikiwa kutoa kiasi cha Bilioni moja na Milioni
750 kama fidia kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mara baada ya kuchukua mradi
wa Halmashauri hiyo ujulikao kama Laki Laki kwa ajili ya kujenga miji ya kisasa
zaidi.
Akidhibitisha mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa
Halmashauri mkurugenzi mtendaji Bw Fidelis Lumato alisema kuwa mpaka sasa
wameshapokea fidia hiyo ya mradi wa mashamba ya Laki laki ambao ulikuwa chini
ya Halmashauri hiyo .
Lumato alisema kuwa pamoja na kuwa mpaka sasa wameshaweza
kuachia mradi huo na kutoa kwa Serikali kuu lakini fidia hiyo itasaidia sana
kuweza kufanya marekebisho ndani ya Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kununua
mahitaji ya msingi.
Alidai kuwa fidia hiyo imeweza kurahisisha kazi mbalimbali
za halmashauri kwa kuwa yapo mahitaji ya msingi ambayo yalikuwa yanahitajika
lakini hapakuwa na jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kununua jambo ambalo
wakati mwingine lilikuwa linasababisha malengo kukwama.
Aidha alitaja vitu ambavyo vitaweza kununuliwa kutokana na
fidia hiyo kuwa ni pamoja na Gari kwa ajili ya matumizi ya shule za sekondari
katika Halmashauri hiyo,tipper kwa ajili
ya shuguli za ujenzi ambapo pia nalo litachangia mapato ya halmashauri hiyo.
Vitu vingine ambavyo vitafanyika kutokana na fidia hiyo ni
pamoja na ukarabati wa jengo la kisasa la Halmashuri hiyo ambalo bado
halijaweza kukamilika rasmi kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri hiyo.
“tunashukuru mungu serikali kutupa fidia ya mradi wa
mashamba ya Lakilaki kwani kwa kipindi cha mwaka huu tutafanya vitu vingi na
tunaimani kabisa hata mapato nayo yataweza kuongezeka zaidi na hivyo kuwasaidia
hata wananchi wenyewe”aliongeza Lumato.
Awali Kaimu Mweka hazina wa Halmashauri hiyo ambaye ni bw Munguabella
Kakulima alidai kuwa kwa sasa Halmashauri hiyo imeweka mikakati mbalimbali ya
kuweza kuongeza vyanzo vya mapato kwani mpaka sasa kuna tofauti kubwa sana ya
ongezeko la mapato katika Halmashauri hiyo ya Arusha Vijijini .
Kakulima alidai kuwa hapo awali waliaanza na mapato ya
Milioni 400 lakini mpaka sasa wameweza kufikia ukusanyaji wa mapato wa zaidi ya
Bilioni 2 jambo ambalo lengo lake ni kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo
inaepukana na tabia ya kuwa tegemezi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment