TANZANIA YAANZA
RASMI KUTUMIA MFUMO WA KIMATAIFA NA KUACHANA NA MFUMO WA ZAMANI
Na
Queen Lema,ARUSHA
Tanzania
imeanza kutumia rasmi mfumo wa kimataifa katika masuala ya ukaguzi wa ndani
ambapo mfumo huo utaweza kupunguza Viashiria mbalimbali vya ubadilifu wa fedha
za umma
Hayo
yamebinishwa leo na mkaguzi mkuu wa ndani hapa Nchini Bw Mohamed Mtonga
wakati akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa ndani kutoka katika kanda ya kaskazini
Mohamed
alisema kuwa mpango huo wa ukaguzi kwa mfumo wa Kimataifa umeanza kutumika
rasmi hapa nchini July Mosi ambapo utaweza kutoa na kuonesha viashiria
mbalimbali ambavyo vinakwamisha shuguli za ukaguzi ndani ya Serikali kuu pamoja
na Serikali za Mitaa.
Alisema
kuwa kupitia mfumo huo mpya wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani utaweza kuboresha
na kuwafanya wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi tofauti
na mfumo uliokuwa hapo awali ambao ulikua hautoi fursa kwa wakaguzi wa ndani
Alifafanua
kuwa hapo awali wakaguzi wa ndani walikuwa wanashindwa kutekeleza
majukumu yao kutokana na viashiria vya vitu mbalimbali kama vile rushwa na
uhusiano baina ya mkaguzi na mkaguliwa hali ambayo ilikuwa chanzo cha
kukwamisha malengo mbalimbali ya ukaguzi hapa nchini ingawaje ndani ya
mfumo wa ukaguzi kimataifa suala hilo halipo kabisa.
Katika
hatua nyingine alisema kuwa wakaguzi wa ndani bado wanakabiliwa na changamoto
ya uhaba wa bajeti hali ambayo nayo inafanya washindwe kufanya kazi na kukagua
miradi kwa wakati husika
Alisema
kuwa kwa sasa wakaguzi wa ndani wanashindwa kufika kwenye miradi tena kwa
wakati kutokana na uhaba wa bajeti ambazo zinatengwa na Halmashauri huku
hali hiyo pia ikichangia sana kutofikia malengo mbalimbali ya kiukaguzi
ambayo yanatakiwa kuwekwa na pia kusaidia jamii
MWISHO
No comments:
Post a Comment