Katika
picha ni Dr. Kandusi akimkabidhi magazeti ya MAN Rais na Mwanzilishi wa
Prostate Health Education Network Ndugu Thomas Ferington. Ndugu
Farrington naye ni manusura, mwathilika na mhanga wa saratani ya tezi
dume.
…………………………………………..
Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi,
manusura, mwathirika na mhanga wa saratani ya tezi dume (prostate
cancer) na mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus campaign akiwa Washington DC
nchini Marekani kwenye Kongamano (Summit) la saratani ya tezi dume
linaofanyika katika jengo la Maseneta wa Marekani Russell Hall Capitol
Hill.
Katika kongamano hilo ambalo
lilihudhuriwa na waathilika na wanaharakati wa saratani ya tezi dume na
baadhi ya Maseneta na Wabunge (Members of Congress) ulijadili pamoja na
mambo mengi umuhimu wa kutoa elimu katika jamii juu ya saratani ya tezi
dume na umuhimu wa kutoa tiba ya kisasa kwa watu wote na mahali popote.
Kongamano liliohudhuriwa na
washiriki takribani mia moja, liliandaliwa na shirika la hiari Prostate
Health Education Network la Marekani na lenye makao makuu huko Boston.
Shirika hilo linakazia “Knowledge is the best defense against prostate
cancer”.
Kongamano liligundua kuwa kwa
kutoa elimu katika jamii utawezesha kupunguza magonjwa ya saratani
(prevention is better than cure) kwa watu wengi. Watu wakielimika na
kupata elimu juu ya hali hatarishi, umuhimu wa kubadili maisha yao kwa
kula vyakula asilia, kufanya mazoezi, kujiepusha na utumiaji wa tumbaku
wa aina yote, kupiga vita unene hatarishi itapunguza sana watu kupata
saratani.
Hii itaokoa nguvu kazi na kuokoa pesa nyingi ambazo zinaweza kutumika kwa maendeleo mengine.