Shirika lisilo
la kiserikali la Hope For Tanzania
limetoa computer 92 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kama mchango wa kuinua kiwango cha elimu katika shule nne
jijini Arusha.
Wakurugenzi wa
shirika hilo
hapa Tanzania Felex Masenge na Naomi Masenge wamesema kuwa msaada huo
unatokana na wafadhili wa shule isiyo ya kiserikali ya Tuishime ambao waliahidi
kuzisaidia shule 10 jijini arusha vifaa hivyo ili wanafunzi waweze
kujifunza somo la Tehama.
Felex amesema
kuwa zoezi hilo
la kupatiwa computer linaendelea hali ambayo itatoa fursa kwa shule hizo
kufanya vizuri kielimu katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Akikabidhi
computer hizo kwa wakuu wa shule hizo ambazo ni shule ya msingi
uhuru,ukombozi,kijenge na tuishime mgeni rasmi katika hafla hiyo
Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa vifaa hivyo vimekuja
wakati muafaka na amewataka kuvilinda na kuvitunza vizuri.
Pia amesema kuwa
shule nyingi za serikali zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha
hali ambayo inapelekea kushindwa kununua computer na
wanafunzi kushindwa kufanya mitihani ya Tehama kama ilivyo kwa
shule zinazomilikiwa na watu binafsi.
Aidha Augustino
ametoa wito kwa wakuu hao wa shule kuzitunza na kuzilinda na kuwa
hatokuwa tayari kupokea taarifa ya kupotea ama kuibiwa kwa vifaa hivyo
bali hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi ya mwalimu husika.
Lakini hata
hivyo amewataka walimu kwenda shule na kwenda kujifunza alimu ya computer ili
waweze kuwafundisha wanafunzi somo hilo la
Tehama na hatimaye waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Akiongea kwa
niaba ya wakuu wa shule diwani wa kata ya sokon one Michael Kivuyo amesema kuwa
ni vyema watanzania wakaiga mfano huo kwa kuchangia kuinua elimu katika shule
za msingi na sio kuchangia ama kutoa msaada kwa mambo yasiyo ya msingi katika
jamii.
Mwisho.
Chanzo cha
habari na Ashura Mohamed Arusha
No comments:
Post a Comment