MHARIRI WA GAZETI LA RAI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA
KUOMBA RUSHWA YA SHILINGI MILIONI 1NA NUSU
Na Queen Lema,ARUSHA
MHARIRI wa gazeti la Rai bw Masiaga Matinyi pamoja na
watuhumiwa wengine wawili wamefikishwa katika mahakama ya Arusha kwa kosa la
kuomba Rushwa kutoka kwa afisa wa Shirika la Tanesco wilayani Monduli mkoani
hapa.
Akisomewa mashitaka pamoja na watuhumiwa wengine wawili
ambao ni bi Bora Bidiga (36)na
Mwita Chomote (32) walitenda kosa hilo
wilayani Monduli
Aidha iliendelea kudaiwa mahakamani hapo mbele ya hakimu
mkazi bw Yohana miombo na mwendesha mashitaka wa Serikal bw Amidu Msimbana kuwa watuhumiwa hao wote walitenda kosa hilo kati ya June 13 na 14
majira ya saa kumi jioni wilayani Monduli Mkoani Arusha
Pia ilidaiwa kuwa watuhumiwa wote hao watatu walimlazimisha
kwa nguvu afisa wa shirika la Tanesco ambaye amejulikana kwa majina ya Andew
Mahamudu kutoa Rushwa kwa kuwa hakuwa na
vigezo vya kufanya kazi ndani ya shirikan hilo
“baada ya kufanya hivyo watuhumiwa wote hawa walimshawishi
awape kiasi cha shilingi Milioni 5 ili wasitangaze lakini baada ya hapo
walipokea kiasi cha shilingi laki mbili ambapo walikamtwa na vyombo vya
usalama”aliongeza bw Amidu.
Aidha iliendelea kudaiwa kuwa Mshitakiwa wa pili ambaye ni
dereva wa mhariri huyo naye anakabiliwa na mashitaka mawili ambapo shitaka la
kwanza ni pamoja na kushawishi kupokea rushwa wakati shitaka la pili ni kupokea
rushwa kiasi cha shilingi laki mbili
“inadaiwa kuwa huyu ndiye alieenda
kupokea kiasi cha shilingi Laki mbili kwa niaba ya Masiaga ambapo kwa kufanya
hivyo ni kosa la kisheria hivyo anakabiliwa na mashitaka mawili ya
kujibu’aliongeza mwendesha mashitaka huyo
Hataivyo watuhumiwa wote watatu
walipewa masharti ya dhamana ambapo walitakiwa kuwa na mdhamini ambaye anafanya kazi katika kampuni
inayofahamika pamoja na kusaini hati ya kiasin cha shilingi laki tano ambapo
wadhamini walifanikiwa kuweka kukidhi matakwa ya mahakama hiyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment