Tuesday, June 5, 2012

WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA,HUYU NDIYE SPIKA WA BUNGE


WABUNGE wa bunge la Afrika mashariki wamemchagua spika wa bunge hilo  kutoka nchini Uganda ambaye ataliongoza bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Spika huyo ambaye ndio mwanamke wa kwanza  kushika wadhifa huo wa juu katika bunge hilo ni  Magreth Zziwa kutoka nchini Uganda mbaye alimbwaga mpizani wake kwa kupata kura 33 dhidi ya   Dora  Byamukama  kutoka  nchini Uganda ambaye alipata kura 12.

Ambapo  awali matokeo ya kura hayakumpa Zziwa nafasi hiyo baada ya kupata kura 27  huku mpinzani  wake kura 18 na kufanya uchaguzi huo kurudiwa upya.

Aidha Mwanamama huyo ataliongoza bunge hilo kuanzia sasa  ni msomi mchumi mwenye shahada ya uzamili wa sayansi ya siasa na uchumi.

Mara baada kuchaguliwa Spika huyo aliapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge hilo ambapo baada ya kula kiapo aliwashukuru wabunge wa bunge hilo kwa kumchagua.

“Naishukuru serikali yangu ya Uganda na pia wananchi wa Uganda na ninyi wabunge kwa kunichagua kushika wadhifa huu nawaomba ushirikiano tuendleze jumuiya yetu”alisema Zziwa.

Mara baada ya zoezi hilo wabunge 45 wa jumuiya waliapishwa rasmi kuwa wabunge wa bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Uchaguzi huo wa spika wa bunge hilo ulihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za afrawali badhin ya ndugu waliokuwa wakifuatilia uchaguzi huo kwa  njia ya luninga zilizofungwa nje ya ukumbi wa bunge hilo walipongeza namna uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Bunge hilo ambalo linazinduliwa kwa mara ya  tatu na kuongozwa na Maspika kutoka nchi wanachama ambao huchaguliwa kwa kupokezana lilianza mwaka 2001 ambapo liliongozwa na SSpika kutoka Tanzani Abdulrahaman Kinana kabla ya kupokelewa na Mkenya anayemaliza muda wake Abdrahin Abdi.

Kazi kubwa ya bunge la afrika Mashariki ni kusimamia na kutunga sheria mbalimbali  za uendeshaji wa mambo katika jumuiya hiyo iliyo mbioni kuwa shirikisho la Afrika mashariki.

No comments:

Post a Comment