HALMASHAURI ya Arusha vijijini Mkoani hapa imefanikiwa kutoa
mafunzo ya kiuasibu pamoja na Stadi za
utunzaji wa vitabu vya mahesabu kwa watendaji wa vijiji 71 ili kuweza kuepusha
halmashaurri hiyo dhidi ya matumizi
mabaya ya fedha hasa vijijini
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
hiyo Bw Khalifa Idda wakati wa kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika Wiki
iliyopita wilayani humo
Bw Idda alisema kuwa hapo awali kulikuwa na kasoro lukuki ambazo zilikuwa zinajitokeza hasa kwa watendaji hali ambayo ilikuwa inasababisha hasara na halmashuri hiyo kushindwa kufikia makusudio ambayo yalikuwa yamelengwa
Alisema kuwa baada ya Halmashauri yake kuanza kuona hali
kama hiyo ililazimika kwa kiwango kikubwa sana
kuhakikisha kuwa wanapuunguza tatizo hilo na
kuanza mpango maalumu wa kutoa elimu hali ambayo imezaa mafanikio makubwa sana
“hapo awali tulikuwa tunashindwa kufikia malengo yetu
mbalimbali kutokana na baadhi yetu kushindwa kuwa na elimu hali ambayo ni chanzo
cha ukwamaji wa miradi mbalimbali lakini kwa sasa mambo yataenda vema
kabisa tofauti na vile ambavyo tulikuwa
hapo awali:”alisema Bw Idda
Pia alibainisha kuwa pamoja na kuwapa elimu hiyo ili wasiwe
chanzo cha kukwamisha malengo mbalimbali pamoja
na Miradi pia jamii hizo za vijijini nazo zitaweza kuwa na manufaa kwa
kuwa watendaji hao sasa wataweza kuandaa mapato na matumizi ambayo hapo awali
hayakuwepo kwa baadhi ya vijiji.
Alisema kupitia mapato na
matumizi pia nao wananchi wataweza kuwa kufuatilia fedha mbalimbali
ambazo zinatolewa na Halmashauri hiyo kwa karibu sana tofauti na hapo awali ambapo wengi
waalikuwa wanaingia katika migogoro kwa kuwa hawajui kuaanda mapato na
matumizi.
Katika hatua nyingine alisema kuwa mpango huo wa kuendeleza
watendaji wa kata na vijiji ni mpango wa kudumu ili kupitia watumishi hao
Halmashauri hiyo iweze kufikia malengo yake ambayo walikuwa wamejiwekea ya
kupambana na changamoto mbalimbali hasa za vijijini
Mwisho
No comments:
Post a Comment