Akikabidhi vitendea kaz i hivyo kwa
wafanyabiashara wa kanda ya kaskazini katika tamasha lililofanyika mjini hapa
meneja wa bia ya safari larger bw Oscar Shelukindo alisema kuwa kampuni hiyo
imejiwekea mpango wa kuhakikisha kuwa wanawasidia wajasiriamali Tanzania nzima
ili waweze kujikwamua katika hali ngumu ya kiumskini.
Alisema kuwa vifaa hivyo walivyovitoa kwa
wafanyabiashara hao ni vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kutumika katika
biashara zao mbali mbali wanazoziendesha kwa kuwa wako watu wana malengo na
maono mazuri ya baishara lakini wanashindwa kufikia malengo kwa ajili ya kukosa
vitendea kazi.
“sisi tumeona tuwe na mpango endelevu wa
kuwasaidia hawa wafanyabiashara vitendea kazi mfano yuko huyu mfugaji wa kuku
tumempatia mashine,mwingine friza ambapo kila mmoja anategemea
biashara anayofanya alimaradi tu wamekidhi vigezo vyetu lazima tumapatie
vitendea kazi “alisema Shelukindo
Aliongeza kuwa zoezi hili litakuwa endelevu
ambapo ametaja kanda ambazo zinahusika na kupatiwa vitendea kazi kuwa ni pamoja
na kanda ya kusini ,mwanza, dares saalam pamoja na kanda ya kaskazini ambapo
aliwataka wafanyabiashara kujitokeza mwaka huu kujaza fomu kwa kuwa endapo
watakidhi vigezo vinavyohitajika nao wataweza kunufaika na vitendea kazi vya
kuendeshea biashara zao.
Awali mgeni rasmi katika tamasha hilo afisa
biashara manispaa ya arusha bw Niarira Elivelema alisema kuwa swala hilo
lililofanywa na Safari Larger ni mfano wa kuigwa na taasisi nyinginezo kwa kuwa
wameonyesha ushirikiano wao na jamii inayowazunguka .
Aliongeza
kuwa endapo wafanyabiashara wadogo watapewa kipaumbele kama walivyofanya tbl ni
wazi kuwa hata taifa nalo litaweza kuongeza kipato kutokana na ushuru ambao
utakuwa unalipwa kutoka kwa wafanyabiashara hao.
mwisho
No comments:
Post a Comment