Na Queen Lema,ARUSHA
WAONESHENI WAHALIFU UPENDO NA PIA WAPENI ELIMU
IMEELEZWA kuwa machafuko ndani ya jamii nyingi yanazidi
kuongezeka kwa kuwa asilimia kubwa ya wanajamii waliowengi wanawatenga wahalifu
mbalimbali badala ya kuwapa elimu ambayo itawafanya waweze kuacha uhalifu wao
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Steve Robert Kutoka Tanga
wakati alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha kwa Muorombo Kata ya Terrat
Mkoani Arusha mapema jana
Bw Robert alisema kuwa kwa sasa hakuna elimu yoyote ambayo
inatolewa kwa watu ambao wanahasi jamii hali ambayo inawafanya hata baadhi yao kutengwa huku uhalifu ukiwa unakithiri sana
Alifafanua kuwa endapo kama jamii ingekuwa na Muongozo imara
hasa katika eneo hilo la Kwa Muorombo basi hata
idadi ya uhalifu nayo ingepungua sana
kwa kuwa kila mara wahalifu wa matukio mbalimbali wangeweza kupatiwa mafunzo
pamoja na madhara ya uhalifu
Alisema kuwa mtu ambaye ni muhalifu hapaswi kutengwa na
jamii yake na badala yake jamii inatakiwa kuonesha na kuimarisha zaidi upendo
ili waweze kufikia katika hatua za kuacha uhalifu ambao ndio chanzo kikubwa sana cha umaskini
“leo hii unakuta eti mtu ni muhalifu lakini badala ya kupewa
elimu mbalimbali ya kumsaidia jinsi ya kuepukana na tabia hiyo anatengwa na
jamii na wakati nafasi mbalimbali zinatakiwa kutumikan ikiwemo nafasi ya
mashirika na Taasisi za Dini”aliongeza bw Robert
Pia aliongeza kuwa wananchi wanapswa kujua mbinu pekee ya
kuweza kukinzana na uhalifu wa aina mbalimbali ndani ya jamii husika ni
kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kuanzia ngazi za familia kwa kuwa nazo familia
nyingi hazina utaratibu wa kuwaelezea watoto wao madhara ya kuwa waharibifu na
wavunjifu wa amani
Awali alitataja madhara ya kukithiri kwa uhalifu hasa wizi
mdogo mdogo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa majanga makubwa sana ya umaskini ndani ya jamii wakati taifa
lina buni mbinu mbalimbali za kupambana na Umaskini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment