Pamela Chilongola na Bakari Kiango.
WANASIASA
nchini, wametakiwa kuacha kujihusishana suala la katiba na badala
yake, suala hilo liachwe mikononi mwa wananchi.Rai hiyo ilitolewa jana
na jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) ,Askofu Dk Alex Malasusa, alipokuwa akizungumza katika
uzinduzi wa Usharika wa Kinyerezi.
Dk
Malasusa alisema katiba ya nchi si mali ya wanasiasa wanaotaka kuiteka
nyara na kwamba hiyo ni mali ya Watanzania, wanaopaswa kupewa uhuru wa
kujadili kwa kina.
Dk
Malasusa alisema wananchi wanapaswa kuwa na fursa kubwa ya kuboresha
mchakato wa kuandika katiba hiyo, lakini wanakwamishwa na asilimia
kubwa ya wanasiasa, wanachangia.
“Sina
ugomvi na wanasiasa katika suala hili, ila naomba wawaachie wananchi,
kwanza ili wapate fursa ya kuchangia maoni yao,” alisema Dk
Malasusa.Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia maoni
yao ili kuboresha katiba inayotarajiwa kuandikwa kwa manufaa ya
wananchi wote.
“Wote
mjitokeze na kutoa maoni yenu, msikae kimya katika mchakato huu,
alisema Dk Malasusa.Pia aliwataka waumini wa kanisa hilo, kubadilika
na kufanya mambo yasiyomchukiza Mungu.Alisema lengi la kanisa hilo ni
kujaribu kuwasaidia waumini wake, ili waweze kubadilika na si
vinginevyo.
No comments:
Post a Comment