STORY NA UPAKO

MKURUGENZI wa halmashauri ya Arusha Vijijini Bw Khalifa Idda amesema kuwa Mpango wa Taasisi ya Aghan wa Kujenga chuo pamoja na hospitali ya Kisasa katika Eneo la Ortument utakuwa ni mpango wenye faida kwa Halmashauri pamoja na jamii kwa kuwa itaweza kupata huduma za afya kwa uraisi tofauti na sasa ambapo wanaenda hadi nje ya mikoa ili kutafuta huduma za afya

Bw Khalifa aliyasema hayo Arusha juzi katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika ndani ya wilaya hiyo 

Alisema kuwa kwa sasa mipango mbalimbali juu ya uwekezaji kutoka katika Taasisi hiyo ya Aghan tayari imeshaanza na mara itakapokamilika basi wataanza ujenzi mara moja kwa kuwa kuwepo kwa Taasisi hiyo ndani ya Halmashauri hiyo kuna tija sana

“napenda kuwaambia wananchi na madiwani wa halmashauri hii kuwa mpaka sasa tuna mpango kama huu ambao kwa kweli kwa haraka haraka sana tunaweza kuona kuwa utaongezea hata halmashauri yetu uchumi wa halmashauri yet”alisema 

Alisema kuwa huu ni wakati wa wanachi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na wawekezaji mbalimbali ili kuweza kuinua na kuboresha maslahi hata ya umma kwa kuwa uwekezaji kama huo ni faida hata kwa jamii
\
Wakizungumza katika baraza hilo madiwani wa halmashauri hiyo walisema kuwa mpango huo ni mzuri sana hasa kwenye ukusanyaji wa mapato na hata kwa huduma za kijamii hasa kwa magonjwa yenye kuitaji wataalamu
Walieleza kuwa wawekezaji hao ambao ni Taasisi ya Aghan wanatakiwa kuhakikisha kuwa kabla ya kuanza ujenzi wao wa chuo kikuu pamoja na Hospitali kubwa sana ndani ya Mkoa wa Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa hawatamdhuru mwananchi yeyote ili wananchi waweze kuwa marafiki wema wa uwekezaji wao

“ni sawa Aghan inakuja kuwekeza hapa lakini tunatakiwa kuhakikisha kuwa uwekezaji wao usiwe ni chanzo cha wananchi wetu kupanda na kushuka na barabara au kumwaga machozi ovyo badala yake uwekezaji wao unatakiwa kuwa mzuri kwa ajili ya maisha yetu sote”walisema Madiwani hao