MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amewataka wataalamu wa Miamba na madini Migodini, kusaidia wachimbaji
wadogowadogo wa madini hususani wa madini ya Tanzanite yaliopo Mererani, Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, kwa kuwapatia mbinu bora na za kisasa za
kufanikisha uchimbaji bora.
Ameyasema jijini Arusha wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Chama cha Wajiolojia Tanzania (TGS), na kuongeza kuwa mbinu bora, zitaleta ufanisi zaidi katika kupata madini bora yatakayoleta tija kuzuaia uharibifu wa mazingira.
Mulongo
alisema kuwa mbali na kufanikisha hayo Pia Jiji litanufaika na
wataalamu hao kukutana Mkoani hapa, kwa sababu wanaamini watapatiwa
utatuzi wa matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkeno na uchafuzi wa maji
unaotokana na kemikali za miamba na gesi za volkeno zinazotokana na bonde la ufa kuupitia mkoa wa Arusha.
Aidha alisema kuwa hivyo ni vema wataalamu hao wakaelimisha wakazi wa Arusha namna bora ya kukabiliana na athari hizo.
Aidha Mulongo alisema ili Tanzania iweze kunufaika na rasiliamli zilizopo kwamanufaa ya Taifa, serikali ya Tanzania iliandaa
mkakati madhubuti wa muda mrefu kwa kusomesha wazawa taaluma
mbalimbali, ili wawe na uwezo unstahili wa kusimamia na kuendeleza
sekta hizo za madini, nishati na maji kwa ufanisi na kwa faida ya nchi
kw aujumla.
Alisema baadhi ya wazawa walionufaika na mkakati huo ni wataalamu wa Wana-jiosayansi ambao wengi wao wamekutana katika mkutano huo, hivyo vema wakaleta changamoto kw
akuelimisha wananchi ili kukuza na kuendeleza sekta hizo ambazo kw
akiasi kikubwa ni baadhi ya mihimili ya uimarishaji wa uchumi na
maendeleo ya kijamii.
Pia
aliomba waibue mikakati ya kukabiliana ipasavyo na majanga ya asili ya
kijiolojia hususani matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkeno na gsi
chafu zitokanazo na vokeno,kemikali zinazotokana kwenye miamba na kuchafua maji, pamoja na mionzi ya asili.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini na Nishati Tanzania, Joseph Kahama, alisema kuwa sekta
hiyo inakabiliwa na changamoto lukuki, lakini kubwa wamejikita
kuzalisha dhahabu na vito vingine kama vile madini aina ya Alili ambayo
inasemekana Tanzania ni ya pili duniani kuw ana madini hayo kwa wingi
Pia changamoto kubwa waliyonayo ni ile ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Madini
ili kuzalisha wataalamu wengi zaidi ya hawa waliopo, lakini hilo
litafanikiwa iwapo serikali itasaidia kusukuma kwa haraka suala hilo.
Alisema kuwa ili hayo yote yafanikiwe kw aharaka, ni lazima serikali kuboresha miundombinu ya reri na barabara iboreshwe ili kurahisisha usafirishaji.
Mwisho
HABARI NA ASHURA MOHAMED ARUSHA
No comments:
Post a Comment