Halmashuri ya manispaa ya jiiji la Arusha inatarajia kupanda
miti zaidi ya 2000 katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo huku lengo halisi likiwa ni kutunza na
kuthamini mazingira .
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Meya wa jiji hilo Gauydence Lyimo
wakati wa zoezi la upandaji miti katika bonde la mto Naura mapema jana.
Lyimo alisema kuwa pamoja na kuwa hii ni wiki ya mazingira
lakini bado kuna jitiada mbalimbali ambazo zinafanywa ili kuweza kuboresha
zaidi jiji la Arusha kwa kuwa yapo maeneo mengi sana ambayo miti yake imekatwa kwa ajili ya
matumizi mbalimbali.
Alifafanua kuwa ili mji wa Arusha ukae katika muonekano
mzuri n Iazima kwanza kuwepo na mpangilio mzuri wa mazingira ambapo mpangilio
huo utaweza kuwanufaisaha hata watanzania hasa wakazi wa Arusha wenyewe.
Alibainisha kuwa mara nyingi zoezi la ukataji wa miti
linakuwa na madhara makubwa sana hasa kwa wakazi
wa mji huu kwa kuwa wanapoteza vitu muhimu ambavyo ni kwa ajili ya maslahi yao wenyewe
Alitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na kukosa maji sanajari na
mvua za uhakika kwa kuwa ambazo ndizo
zinazozalisha vyakula kwa mpangilio hali ambayo wananchi wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanajifunza kutokana na hali ya ukame ambayo inaikumba baadhi ya familia
Awali alisema kuwa mbali na hayo yote pia nayo makampuni
mbalimbali yanatakiwa kuhakikisha kuwa yanaboresha mji wa Arusha kwa kupanda
aina mbalimbali za miti ambazo zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuboresha hata uoto
wa asili
Aliyataka makampuni yote hata kama ni makampuni ya Kitalii
kujiwekea utaratibu na kama makampuni yote ndani ya Jiji hilo
watapanda miti pembezoni mwa jiji basi huenda hali ya jiji ikarudi kama ilivyokuwa hapo awali.
No comments:
Post a Comment