HII NI MOJA YA PICHA YA WATOTO WA MITAANI WAKIWA WAMELALA NDANI YA MAENEO MBALIMBALI YA NCHI YA TANZANIA
STORY NA UPAKO WA HABARI
WATOTO wanaoishi
mazingira magumu na hatarishi ndani ya Stendi ya mabasi yaendayo Mikoani Mjini
Arusha wameomba Serikali na Mashirika mbalimbali kuwasaidia kwa kuwa wapo
baadhi ya watu wazima ambao wanataka kuwaingilia kinyume cha maumbile kwa
kisingizio kuwa ni watoto wasio na waangalizi
Hayo yamebainishwa na
watoto hao wakati wakiongea na “UPAKO WA HABARI”katika eneo la pembezoni mwa Stendi ya
mabasi yaendayo Mikoani ndani ya Jiji la Arusha mapema jana.
Wakizungumzia Tatizo hilo watoto hao walisema kuwa wanalazimika kuogopa sana hasa nyakati za usiku kwa kuwa wapo baadhi ya watu
wazima ambao wanawataka kinyume cha maumbile na kudai kuwa watawapa fedha
ambazo ni kati ya 1000- 2000 mara baada
ya kufanya tendo hilo
Walisema kuwa hali hiyo inawatisha sana na kuwafanya wengine kukosa amani hasa
nyakati za usiku kwa kuwa wanapokataa kufanya matendo hayo hulazimika kupigwa
na hata mara nyingine watu hao wazima kuwaambia watoto wenzao kuongeza kipigo
“huwa tunaogopa sana
hata kujilaza katika mitaro kwa kuwa hawa watu ambao ni kama baba zetu na
wengine kama babu zetu wanapokuja kutuomba kufanya nao tendo hilo sisi
tunakataa kwa kuhofia kuumia na hata kupata Ukimwi sasa tunaomba Ushirikiano
uwepo baina yetu sisi na Polisi watakapokuja tu washikiliwe kwa kuwa hata sisi
tunahaki ya kuishi”walisema watoto hao
Wakati huohuo watoto
hao waliiomba wamiliki wa vyoo hasa katika maeneo ya stendi hiyo kuwasaidia
kuwapa huduma za vyoo bure kwa kuwa wanalazimika kutumia mifuko midogo na kisha
kujisaidia haja kubwa hali ambayo ni hatari hata kwa afya zao
Watoto hao waliongeza
kuwa hali hiyo mbali na kuwa ni hatari kwa afya zao pia inachafua hata hali ya
usafi wa jiji kwa kuwa wanalazimika kutupa vinyesi hivyo kwenye barabara kuu za
jiji la Arusha huku Mji wa Arusha ukiwa unapiga kelele za usafi
“tunapowaomba
wamiliki wa vyoo watusaidie tuweze kujisaidia hata haja ndogo wanatukatalia
badala yake wanatuambia kuwa tuwe na 200
sasa kama hakuna mtu aliyetupa siku hiyo
tunatumia mifuko na kisha tunatupa vinyesi hivyo bila hata mpangilio maalumu”walisema watoto hao
MWISHO
No comments:
Post a Comment