TANZANIA
imefanikiwa kuvuna pamba kilo millioni 224
kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 wakati katika msimu wa miwaka
2010/2011 kilo Milioni 163 ziliweza kuvunwa kwa mwaka hali ambayo
imefanya zao hilo kuongeza thamani ya zao hilo zaidi kwa wakulima
katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yameelezwa na Bw Marko Mtungu ambaye ni Mkurugenzi wa
bodi ya pamba hapa nchini wakati akiongea na wadau mbalimbali wa zao la pamba
mapema jana jijini hapa.
Bw Marko alisema kuwa ongezeko hilo
la kilo za pamba linatokana na juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na wadau wa
zao hilo kwa
kushirikiana na nchi nyingine za Afrika hali ambayo imeonekana kuzaa matunda.
Aidha aliongeza kuwa kuongezeka kwa mavuno kwa zao hilo la
pamba pia kumekuwa na faida kubwa sana kwa wakulima wa zao hilo kwa kuwa wameweza kufanya zao hilo la Pamba kuwa na
thamani hali ambayo nayo imechangia kwa kiwango kikubwa sana kuongezeka hata
kwa ulimaji, na mauzo.
“kwa sasa nchi hii
imeweza kupata mavuno mengi sana kutokana na juhudi mbalimbali lakini pamoja na
hayo yote pia kama jitiada zitaongezwa ni zaidi kuwa zao hili litaweza
kuzalishwa kwa hali ya juu sana tofauti na sasa’alisema Bw Marko.
Hataivyo alitaja Nchi ambazo zinaongoza kwa kulima sana
pamba kuwa ni pamoja na Nchi ya Tanzania ikifuatiliwa na nchi ya Zimbabwe
wakati kwa upande wa mikoa ni Mkoa wa Shinyanga.
Naye Mkurugenzi wa shirika la viwango hapa nchini(TBS) bw Charles
Ekelege alisema kuwa ili kufanya zao hilo la Pamba liwe na ubora wa kimataifa
wakulima wa zao hilo wanapswa kuhakikisha kuwa wanatumia na kufuata utaratibu
wa kuhakikisha kuwa wanatumia maabara za upimaji wa zao hilo
Bw Ekelege aliongeza kuwa kwa kutumia utaratibu wa kupima
zao hilo utaweza kuwafanya watanzania walima zao
hilo kuuza kwa
ubora ambao unatakiwa katika masoko mbalimbali ya dunia.
‘ili hili zao la pamba liweze kuwa katika viwango vya
kimataifa ni lazima kwanza walimaji wa zao hilo kuhakikisha kuwa wanapima ubora
wa zao hili kwa kutumia njia za kisasa zaidi na wala sio kwa kutumia njia za
macho kwani njia hizi za macho zinachangia sana wakulima kuuza mazao yao bila
kuwa na bei maalumu hasa katika masoko ya kimataifa kwa kuwa pale wanaambiwa
kuwa wauze kwa bei yoyote’aliongeza bw Ekelege.
Katika hatua nyingine alisema kuwa watanzania wanatakiwa
kujiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanapima na kutoa ubora wa mazao yao kabla ya kuingiza sokoni hali ambayo itachangia kwa
kiwango kikubwa sana
kukuza hata uchumi wa nchi.
Nao
wadau mbalimbali wa zao hilo la pamba walisema kuwa pamoja na kuonekana
kukuwa kwa kiwango cha uvunaji wa zao hilo la pamba lakini bado kuna
umuhimu mkubwa sana wa Serikali kuhakikisha kuwa inatatua matatizo
ambayo yapo kwenye zao hilo kwa kuwa bado kuna uwezo kuongezeka kwa
mavuno katika zao hilo
HABARI NA UPAKO WA HABARI
No comments:
Post a Comment