MWENYEKITI WA UMOJA WA SHULE BINAFSINA VYUO BINAFSI BI ESTER LEMA AKINENA JAMBO
WADAU WAKIFUATILIWA KWA UKARIBU SANA
HABARI NA UPAKO WA HABARI
WAMILIKI wa shule binafsi wametakiwa kuacha kutoa ajira
zaidi kwa walimu wa mataifa ya nje na badala yake wachukue walimu wa kitanzania
ambao wanauwezo ili kuepusha shule zao na udanganyifu wa mithiani
Kauli hiyo imetolea mjini hapa na afisa elimu wa manispaa ya
Arusha Bw Omary Mkombole wakati akiongea na wanachama wa Tamongsco ambao ni
wamiliki pamoja namameneja wa shule mbalimbali jijii hapa
Bw Mkombloe alisema kuwa wamiliki hao wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanajiamini katika kazi zao ili waweze kufikia malengo mbalimbali ambayo
wanayatka lakini kama wataendelea kuwathamini zadii walimu wa mataifa ya nje
basi hawataweza kufikia malengo
Alisema kuwa kuongeaz kingereza kwa mwalimu isiwe ni tija
mojawapo ya kusababisha asilimia kubwa ya watu kuweza kuajiriwa bali wanatakiwa
kuangalia sifa na vigezo vya mwalimu bora
Wakati huo huo mkaguzi wa elimu kanda ya kaskazini magharibi
bw Victor Bwindiki aliwaambia walimu hao kuwa wanatakiwa kuwa wabiunifu dhidi
ya shule zao za binafsi ili wali mu wasiwakambie ovyo
Bwindiki alisema kuwa endapo kama wamiliki wa shule
wataboresha taasisi zao basi itasaidia kwa kiwango kikubwa sana
hata kuweza kuongeza idadi ya wasomi ndani ya nchi ya Tanzania
Awali wamiiki hao wa shule pamoja na mameneja walisema kuwa
wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kuweza
kuwafikia wananchi kwa kuwapa elimu iliyo baora lakini kinachowasumbua ni
utozwaji wa kodi kubwa sana
Akiongea kwa niaba ya
wakuu hao mwenyekiti wa umoja huo jijini hapa Bi Ester Lema alisema kuwa
Serikali inatakiwa kuaangalisa shuguli ambazo wanazifanya kwani ni shuguli
kubwa sana ya
kuweza kusadiia jamii lakini bado Serikali hiyohiyo imekuwa ni chanzo mojawapo
cha kuwatoza ushuru.
Mwisho
No comments:
Post a Comment